Wanachama wa chama Cha Moyo Mtakatifu wa Yesu Parokia ya Shinyanga mjini, wamejitokeza kwa wingi kwenye Misa ya kumwombea Mwanachama mwenzao Bi. Editha Edward, iliyofanyika leo katika Kanisa la Moyo safi wa Maria Parokia ya Shinyanga mjini, kabla ya Mazishi ambayo yanafanyika katika makaburi ya Nguzonane mjini Shinyanga.
Bi. Editha Edward aliyekuwa maarufu kama Mama Taska, alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Bugando Jujini Mwanza siku ya Jumatatu tarehe 08.04.2024.
Enzi za uhai wake Bi. Editha alifanya majitoleo mbalimbali katika Kanisa Parokia ya Shinyanga mjini, ikiwa ni pamoja na kwenye chumba kuandaa mavazi ya Mapadre kwa ajili ya Misa (Sacrastia)
Bi. Editha ambaye pia amekuwa Mwanachama wa Shirika la wazee na wastaafu katika Parokia ya Shinyanga mjini na kushika nafasi mbalimbali katika uongozi wa Jumuiya, alizaliwa mnamo mwaka 1941, huko Bukoba mkoani Kagera.
Mungu ailaze roho yake mahali pema Mbinguni...Amina.
Post a Comment