" BABA MTAKATIFU FRANCISCO AELEZA KUSIKITISHWA VIFO VYA WAFANYAKAZI SABA GAZA

BABA MTAKATIFU FRANCISCO AELEZA KUSIKITISHWA VIFO VYA WAFANYAKAZI SABA GAZA

 Baba Mtakatifu Francisco  ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya wafanyakazi saba wa mashirika ya kutoa misaada waliouwawa kwenye  mashambulizi ya Israel huko Gaza

Akizungumza wakati wa hotuba yake ya kila wiki Baba Matakatifu Fransco  ameziombea familia za wafanyakazi hao na kutoa wito wa njia za uwasilishwaji misaada kwa watu wa Gaza, kufunguliwa na kuachiwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas.

Wito huu wa Papa Francis unakuja wakati ambapo Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk akisema  kuwa, shambulizi hilo la Israel limevuruga mahusiano ya nchi hizo mbili na kwamba Israel inauweka uungaji mkono wa Poland kwake katika mtihani mkubwa.

Hayo yanafanyika wakati ambapo wizara ya afya ya gaza inayoendeshwa na kundi la Hamas, imesema kufikia sasa Wapalestina karibu 33,000 wameuwawa kutokana na mashambulizi ya Israel.

Post a Comment

Previous Post Next Post