" DC MHITA AHIMIZA WAWEKEZAJI WA MADINI KAHAMA KUTOA FURSA ZA AJIRA KWA WAZAWA

DC MHITA AHIMIZA WAWEKEZAJI WA MADINI KAHAMA KUTOA FURSA ZA AJIRA KWA WAZAWA


Na Sebastian Mnakaya, Kahama

MKUU wa wilaya ya Kahama Mhe.MBONI MHITA amewataka wawekezaji wa madini wilayani humo kushirikiana na jamii inayowazunguka katika kutoa fursa za ajira kwa wazawa pamoja kusaidia shughuli za kijamii ikiwemo kusaidia kujenga shule, ujenzi wa barabara, uchimbaji wa visima pamoja na zahanati.

Mhe. MHITA ameyasema hao wakati alipotembelea kiwanda kidogo cha kuchakata madini cha LEONARD BARNAB RUCHAGULA kilichoopo kijiji cha Ilelema kata ya Shilela katika halmashauri ya Msalala, ambapo amesema kuwa uwekezaji hautakuwa na maana kama hautaweza kuwanufaisha jamii inayowazunguka migodi hiyo ili kuendelea kupunguza migogoro mbalimbali katika maeneo hayo kwa kuwa na ushirikiano.

Naye, msimamizi wa kiwanda hicho PAUL JACKSON amesema tangu kuanzishwa kwa mradi huo, wameweza kuzalisha kiwango cha dhahabu chenye uzito wa gramu 11,876 wenye thamani ya Bilioni 2 za kitanzania, huku wakiendelea kushirikiana na wananchi wa eneo hilo kwa kusaidia kwa kujengwa kwa Zahanati pamoja na kusaidia ujenzi wa barabara.

Kwa upande wake diwani wa kata ya Shilela FILIBETH MPINA, amesema kuwa uwekezaji huo amekuwa na ushirikiano na wananchi katika eneo hilo kwa kusaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye kata hiyo ambapo ameomba   waendelee hivyo na pasipo kuchoka ili wananchi waendelee kunufaika na uwekezaji huo.

Baadhi ya wananchi wa kijiji cha Ilelema katika kata ya Shilela MATRIDA SALIBOKO na JOHN KABINI wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wanawashukuru wawekezaji kwa kuwekeza katika kijiji hicho, ambapo umeweza kuwasaidia kupata ajira kwa vijana wao pamoja na kuendelea kujenga miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mbona Mhita, katikati akiendelea na ziara yake.










Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita akiwa kwenye picha ya pamoja.


Post a Comment

Previous Post Next Post