" MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA WAKILI JULIUS MTATIRO AAHIDI KUENDELEA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA WELEDI NA UADILIFU

MKUU WA WILAYA YA SHINYANGA WAKILI JULIUS MTATIRO AAHIDI KUENDELEA KUWAHUDUMIA WANANCHI KWA WELEDI NA UADILIFU

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro ameendelea na ziara yake kusikiliza, kupokea na kuratibu utatuzi wa kero za wananchi.

Wakili Julius Mtatiro leo April 03,2024 amesikiliza kero za wananchi katika tarafa ya Shinyanga Mjini kupitia Mkutano wa hadhara uliofanyika katika eneo la soko kuu,  ambapo wananchi wamewasilisha kero na malalamiko mbalimbali ikiwemo migogoro ya ardhi pamoja na ubovu wa miundombinu ya Barabara.

DC Mtatiro amesema kwamba serikali Wilayani  Shinyanga itahakikisha inaendelea kuhudumia wananchi kwa weledi na uandilifu.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria Mkutano huo wa hadhara wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro kwa kutoa nafasi ya kusikiliza kero zinazowakabili wananchi,hali wanayoitaja kuwa ni uongozi  thabiti uliotukuka

Mkutano wa hadhara uliofanyika   jioni,  umetanguliwa na kikao cha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga na makatibu tarafa pamoja na maafisa watendaji  wa kata wa  halmashauri mbili za wilaya hiyo,kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa ya Shinyanga,wa Lewis kalinjuna ambapo pamoja na kuwapongeza lakini amewataka kuendelea kuwahudumia  wananchi kwa weledi na uadilifu huku akisisitiza zaidi uwajibikaji.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Wilaya hiyo ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Wakili Julius Mtatiro akizungumza kwenye mkutano wake wa hadhara na wananchi wa Wilaya hiyo ambao umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa chama cha mapinduzi CCM Wilaya ya Shinyanga.

Viongozi mbalimbali wa serikali na chama cha mapinduzi CCM.




Post a Comment

Previous Post Next Post