Na Elisha Petro
Klabu ya Bayern Munich imetupwa nje katika michuano ya UEFA champions league kwa jumla ya goli 4-3 hatua ya nusu fainali kufuatia kichapo cha goli 2-1 dhidi ya wenyeji wao Real Madrid, ikumbukwe kuwa mchezo wa mkondo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya 2-2.
Alphonso Davies alianza kufufua matumaini ya Bayern Munich kutinga hatua ya fainali dakika ya 68 lakini jitihada hazikuzaa matunda baada ya Joselu aliyeingia dakika 81 kuisawazishia Real Madrid dakika ya 88 na kisha dakika ya 90+1 yule yule super sub Joselu akaifungia Real Madrid goli la pili lililowapeleka hatu ya fainali ya Michuano hiyo.
Real Madrid watavaana na Borussia Dortmund katika hatua ya fainali kwenye uwanja wa Webley wenye uwezo wa kubeba mashabiki elfu 90 uliopo nchini Uingereza , kumbuka Dortmund waliotinga fainali hiyo baada ya kuitamatisha safari ya PSG kwa jumla ya magoli 2-0 baada ya ushindi wa goli 1-0 nyumbani na ugenini.
Fainali itachezwa 01/06/2024 nani kutwaa ubingwa wa klabu bingwa barani ulaya ( UEFA Champions league) msimu wa 2023/2024.

Post a Comment