Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI WAPONGEZA UWEPO WA WIKI YA MAZIWA


Baadhi ya Wadau Mkoani Mwanza wamepongeza Bodi ya Maziwa Kwa kuandaa tukio la wiki ya Maziwa ambalo linafanyika katika Viwanja vya Furahisha Mkoani humo.

Akizungumza na Misalaba Media, Meneja Mkazi wa Urus Tanzania Ltd amesema wao kama Kampuni uwepo huu wa Wiki ya Maziwa utasaidia kuweza kuongea na Wafugaji Moja Kwa moja kuwapa Elimu Namna ya kutumia vifaa Sahihi vya Namna ya kufuga Kwa Njia ya kisasa

Naye pia msajili wa Maziwa Nchini (TDB) Profesa George Msuya alisema wiki ya Maziwa Kitaifa Uwanja wa Furahisha Wilaya ya Ilemela Mkoani Mwanza kauli Mbiu ni "kunywa Maziwa Salam Kwa Afya Bora na uchumi endelevu yaliyoanza mei28 Hadi Juma Moss Mwaka huu

"Maziwa yanasaidia kujenga uchumi wetu Lazima tuyatangaze kwani Yana Mchango Mkubwa wa kujenga uchumi wa Nchi na ajira ambapo Lita 100 zinatoa ajira za kudumu Kwa watu wa nne.




Post a Comment

0 Comments