Watu watatu wa familia moja Mama na watoto wawili wamefariki Dunia wakati wakipatiwa matibabu katika kituo cha Afya cha Negezi tarafa ya Negezi Wilayani Kishapu baada ya kula chakula kinachosadikiwa kuwa na sumu.
Taarifa hiyo imetolewa na kaimu kamanda wa Jeshi la
Polisi Mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Kenedy Mgani wakati akizungumza na Misalaba
Media ofisini kwake.
Amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia jana
Jumatatu Julai mosi, katika kitongoji cha Nyangalu, kijiji ca Mwajiginya A,
Wilayani Kishapu ambapo Mama na watoto
hao wawili walikula chakula cha usiku lakini baadaye walianza kujisikia vibaya
hali iliyowalazimu kuwahishwa kwenye kituo cha Afya cha Negezi kwa ajili ya matibabu, lakini
walifariki Dunia wakati wakipatiwa matibabu.
Ameeleza kuwa Uchunguzi zaidi unafanyika ili kubaini
chanzo cha tatizo lililosababisha vifo vya wanafamilia hao watatu,na wengine
wanne ambao wanaendelea na matibabu.