" BILA VIBOKO INAWEZEKANA SHULENI

BILA VIBOKO INAWEZEKANA SHULENI

KUTOKUTOA adhabu ya viboko kwa wanafunzi ni njia mojawapo inayosisitizwa katika malezi kwa watoto wawapo shuleni ili kuwawezesha kuwa karibu na walimu hivyo kusaidiwa vizuri katika kufikia malengo yao ya elimu.

Wito huo umetolewa Jijini Mwanza na Mkurugenzi wa shule ya Vikitoria English Medium Switbertus Tibandekile akisema hatua imewezesha shule yao kuwa na wanafunzi wenye tabia nzuri na kufanya vizuri kwenye masomo yao shuleni hapo.

"Sisi kwenye shule yetu tuna kauli mbiu tunayosema Nidhamu Chanya bila Shinikizo la viboko" alisema Tibandekile.

Alisema hatua hiyo inasitahili kuungwa mkono kwani  imewafanya wanafunzi wao wafaulu vizuri kwenye mitihani yao wanayofanya.

Meneja Masoko na Mahusiano kwa wateja wa benki ya CRDB tawi la Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agostino (SAUT) Jovitha Kyaruzi alisema kiwepo kwa Mahusiano mazuri baina ya walimu na wanafunzi ni njia nzuri ya kuwawezesha watoto wafurahie masomo yao na kuwa na fursa ya kudadisi vitu vizuri.

Alisema kumekuwepo kwa imani kuwa mtoto anatakiwa achapwe viboko anapokosea lakini hiyo si njia sahihi ya kumjenga mtoto kwani hatua hiyo wakati mwingine imekuwa ikichangia unyanyasaji kwa kundi Hilo la watoto.

Kyaruzi alisema kunapokuwa na mazingira ya urafiki baina ya walimu na wanafunzi ni njia chanya ya kuwezesha kundi hilo kuwa upendo wa masomo wanayofundishwa. 

Aidha aliwataka vilevile wazazi kuwa karibu na watoto wao wawapo nyumbani na kuepuka sababu ya kuwa na shughuli nyingi hivyo kushindwa kuzungumza nao ili kuwajengea maadili mema.

Mzazi ambaye mwanaye anamaliza darasa la saba katika shule hiyo Ruth Nyanda ambaye ni Mdhibiti Ubora wa Elimu Kanda ya Ziwa alisema amevutiwa na shule hiyo kwa kutokuwa na chembe zozote za unyanyasaji watoto kwa vipiho vya viboko.

Post a Comment

Previous Post Next Post