Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya NYUNDO FC imefanikiwa kutinga hatua inayofuata
ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuiondoa NZOZA FC kwa mikwaju ya
penati kufuatia mchezo wa leo Jumapili Mei 31, 2026 ambapo umemalizika bila
kufungana ndani ya dakika 90 za kawaida.
Mchezo huo uliochezwa katika uwanja wa Mwabenda kata
ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ulikuwa na ushindani mkubwa huku
timu zote zikitengeneza nafasi mbalimbali za kufunga lakini zikiwa
hazikufanikiwa kuzitumia ipasavyo.
Baada ya dakika 90 kumalizika kwa sare ya 0-0, sheria
za mashindano zilihitaji mshindi kupatikana kwa mikwaju ya penati ambapo NYUNDO
FC ilionesha utulivu mkubwa na kufanikiwa kushinda kwa penati 5-3.
Katika hatua hiyo, NZOZA FC ilikosa penati moja muhimu
iliyowagharimu nafasi ya kuendelea na mashindano hayo, huku NYUNDO FC ikitumia
vizuri nafasi zake zote na kufuzu hatua inayofuata.
Kutokana na ushindi huo, NYUNDO FC sasa itasubiri
mshindi wa mchezo wa kesho ili kujua mpinzani wake katika hatua inayofuata ya
mashindano hayo yanayoendelea kuvutia timu na mashabiki kutoka ndani na nje ya
Mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Makamu Mwenyekiti wa
NIACHEKONA CUP, Bwana Samwel Stephen ametangaza ratiba ya mchezo wa kesho
ambapo MAWEMIRU FC itamenyana na MAHEMBE FC katika pambano linalotarajiwa kuwa
na ushindani mkubwa.
Ameendelea kuwahimiza wananchi, wadau wa michezo
pamoja na mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda ili
kuendelea kushuhudia vipaji vya vijana pamoja na burudani ya soka inayotolewa
kupitia mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul
Daud Augustino (MC NIACHEKONA) kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation kwa
lengo la kuibua vipaji vya vijana, kuimarisha amani na kukuza michezo katika
jamii.
Kwa huduma za ushereheshaji wa matukio mbalimbali,
matangazo na burudani, MC NIACHEKONA anapatikana kupitia namba 0757 267 738.
Kikosi cha Nzoza FC.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








































Post a Comment