Vyama vya ushirika Mkoani Ruvuma vimetakiwa kuongeza thamani ya mazao kupitia usindikaji, kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi kwa lengo la kuinua uchumi wa wakulima Akizungumza wakati wa kufunga jukwaa la 6 la maendeleo ushirika (JUMRA) uliofanyika ukumbi wa wa Chuo cha ufundi stadi (VETA) wilaya ya Nyasa,Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed amewataka wadau na viongozi wa vyama vya ushirika kuendelea kufanya kazi kwa umoja, kuongeza thamani ya mazao kupitia usindikaji, kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia na elimu ya ushirika kwa wanachama.Pia,amewapongeza waandaaji wa jukwaa hilo kwa kuendelea kuwaunganisha wanaushirika na kuwapatia elimu muhimu itakayosaidia kukuza ushirika na uchumi wa wanachama. Amesisitiza vyama vya ushirika kutumia fursa zinazotolewa na Serikali, hususan katika sekta ya kilimo, ili kujenga ushirika imara na wenye tija.Aidha, alikabidhi madawati 20 yenye thamani ya shilingi milioni 2 yaliyotolewa na JUMRA kwa Shule ya Msingi Litui..SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment