Picha ya Daniel Patrick Kapaya
Katibu wa Jumuiya ya Shujaa wa Maendeleo na Ustawi wa Jamii Tanzania (SMAUJATA) Mkoa wa Shinyanga, Shujaa Daniel Kapaya, ameteuliwa kuwa Katibu wa SMAUJATA Kanda ya Ziwa.
Uteuzi huu umefanywa na Mwenyekiti wa Taifa wa SMAUJATA, Shujaa Sospeter Mosewe Bulugu, na unanza rasmi leo, tarehe 23 Agosti 2024.
Katika wadhifa wake mpya, Shujaa Kapaya atahudumia mikoa ya Shinyanga, Mwanza, Geita, Kagera, Simiyu, na Mara.
Awali, alihudumu kama Katibu wa SMAUJATA Mkoa wa Shinyanga, ambako alijipambanua kwa juhudi zake katika kuendeleza ustawi wa jamii na kuimarisha mshikamano miongoni mwa wanajumuiya wa SMAUJATA.
Uteuzi huu unampa Shujaa Kapaya jukumu kubwa zaidi la kusimamia na kuratibu shughuli za SMAUJATA katika mikoa yote ya Kanda ya Ziwa, akiongoza juhudi za kuleta maendeleo na ustawi wa jamii katika eneo hilo.
SMAUJATA ni jumuiya ya kitaifa inayopinga ukatili nchini, ikitekeleza majukumu yake chini ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, inayoongozwa na Dkt. Dorothy Gwajima.
Jumuiya hii inasaidia serikali kupitia maafisa wa ustawi wa jamii na maendeleo ya jamii, pamoja na kushirikiana na Jeshi la Polisi kupitia Dawati la Jinsia ili kuhakikisha wahanga wa ukatili wanapata msaada wa haraka na haki inatendeka.
Kauli mbiu ya SMAUJATA, "KATAA UKATILI WEWE NI SHUJAA," inaendelea kuakisi dhamira ya jumuiya hii katika kujenga taifa lenye mshikamano na maendeleo endelevu.
Endelea kutembelea MISALABA MEDIA kila wakati.
Post a Comment