Na Mapuli Kitina Misalaba
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa
Shinyanga wamewashukuru wananchi kwa kuwapa ushindi wa kishindo katika uchaguzi
wa Serikali za Mitaa, Vijiji, na Vitongoji uliofanyika hivi karibuni.
Kwa mujibu wa katibu Siasa, Uenezi na Mafunzo Mkoa
wa Shinyanga Bwana Richard Raphael Masele, chama hicho kimefanikiwa kupata
ushindi wa asilimia 100 katika mitaa 90 ya mkoa huo. Katika vijiji 506, CCM
imeshinda vijiji 504, ikilingana na asilimia 96.6 ya ushindi. Aidha, chama
hicho kimepata ushindi wa asilimia 99 katika vitongoji 2,703, kwa kushinda
vitongoji 2,666.
Masele ameeleza kuwa ushindi huo utaimarisha juhudi
za chama hicho katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kijamii na kiuchumi.
CCM imeahidi kuendelea kushirikiana na wananchi
kuhakikisha kuwa ahadi zote zilizotolewa wakati wa kampeni zinatekelezwa
kikamilifu kwa ustawi wa Mkoa wa Shinyanga.

Post a Comment