" MAHAFALI YA PILI YA ANGLE GABRIEL DAY CARE: WATOTO 24 WAHITIMU KWA FURAHA, JONATHAN MANYAMA KIFUNDA AKIPONGEZA KITUO KWA MALEZI BORA YA KIZALENDO

MAHAFALI YA PILI YA ANGLE GABRIEL DAY CARE: WATOTO 24 WAHITIMU KWA FURAHA, JONATHAN MANYAMA KIFUNDA AKIPONGEZA KITUO KWA MALEZI BORA YA KIZALENDO

 Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa, Jonathan Manyama Kifunda, amepongeza uongozi wa Kituo cha Angle Gabriel Day Care kilichopo Mwasele, Manispaa ya Shinyanga, kwa juhudi zao kubwa za kizalendo katika kusimamia makuzi na malezi ya watoto kupitia elimu.Akizungumza kama mgeni rasmi wakati wa mahafali ya pili ya kituo hicho, Kifunda amewataka wazazi na walezi kutumia fursa hiyo kupeleka watoto wao katika kituo hicho kwa malezi bora na mafunzo muhimu yanayochochea maendeleo ya watoto.“Niupongeze uongozi wa Angle Gabriel Day Care ukiongozwa na Mkurugenzi Bi. Damary Jilungu Mollessi. Huyu dada anafanya kazi hii kwa moyo wa kizalendo na kwa utaalamu mkubwa, akitumia shahada yake ya Saikolojia kuboresha malezi ya watoto. Niwaombe wazazi na walezi tumtumie huyu dada na kituo chake, kwani kinatoa mafunzo yanayowaandaa watoto wetu kwa maisha yao ya baadaye,” amesema Kifunda.Aidha, amemuomba Mkurugenzi wa kituo hicho kuendelea kuwa na moyo wa upendo na kujitolea zaidi katika kuwahudumia watoto wanaojiunga na kituo hicho.“Nikuombe Bi. Damary uendelee kuwa na moyo wa upendo na kujitolea. Hakikisha unawapokea na kuwalea watoto wote wanaojiunga hapa ili wazazi na walezi waone thamani ya kituo chako,” ameongeza.Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Angle Gabriel Day Care, Bi. Damary Jilungu Mollessi, amewahakikishia wazazi na walezi kuwa kituo hicho kinaendelea kutoa malezi na elimu bora kwa watoto.“Niwaombe wazazi na walezi muendelee kukiamini kituo hiki. Tutawalea watoto wenu kwa maadili, kiroho, kimwili, kiakili, na kijamii. Tunawajengea uwezo wa kujieleza, kushughulikia changamoto, na kuwafundisha masomo muhimu kama hesabu, lugha, elimu ya mazingira, sanaa, michezo, na ulinzi wa uhakika,” amesema Bi. Damary.Katika mahafali hayo baadhi ya wazazi na walezi wametoa pongezi kwa uongozi wa kituo hicho kwa malezi mazuri na elimu inayoongeza uwezo wa watoto kufikiri na kuwaandaa kwa shule ya msingi.Mahafali hayo yamewashirikisha wanafunzi 24 waliomaliza malezi yao ya miaka mitatu katika kituo hicho, wakiwemo wavulana 14 na wasichana 10. Hii ni mahafali ya pili tangu kuanzishwa kwa kituo hicho.Karibu ANGEL GABRIEL DAY CARE kwa malezi Bora ya mtoto wako. Michezo ndani na nje, mazingira Bora ya kujifunzia, usalama wa uhakika, usafiri upo. Asante kwa kuwasiliana nasi karibu sana.Wasiliana nasi 0752516752/ 0675969213Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Manyama Kifunda akizungumza kwenye mahafali ya pili katika kituo cha Angel Gabriel Day Care Novemba 30, 2024 Manispaa ya Shinyanga
Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Shirika la Thubutu Africa Initiatives Jonathan Manyama Kifunda akizungumza kwenye mahafali ya pili katika kituo cha Angel Gabriel Day Care Novemba 30, 2024 Manispaa ya Shinyanga
Mkurugenzi wa kituo cha Angel Gabriel Day Care Bi. Damary Jilungu Mollessi akisoma taarifa ya kituo chake  katika mahafali hayo Novemba 30, 2024.





 

Post a Comment

Previous Post Next Post