Na Mapuli Kitina Misalaba
Mashindano ya Krismas Cup yanayoendelea katika
Kijiji cha Salawe, Wilaya ya Shinyanga Vijijini, yamezidi kuonyesha ushindani
mkubwa baada ya mechi ya leo kati ya Machongo FC na Mwabenda FC kumalizika kwa
matokeo ya kusisimua.
Mechi hiyo imeanza kwa kasi huku Junior wa Machongo
FC akifunga bao la kwanza dakika ya 14 na kuipa timu yake uongozi wa mapema.
Hata hivyo, Mwabenda FC imesawazisha kupitia penalti iliyofungwa na Sylvester
dakika ya 45, na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika
90.
Baada ya sare hiyo, mshindi ameamuliwa kwa mikwaju ya
penalti ambapo Mwabenda FC imeibuka kidedea kwa ushindi wa penalti 4-2, hivyo
kusonga mbele katika mashindano haya yenye ushindani mkubwa.
Mgeni rasmi wa mechi ya leo Disemba 1, 2024 ni Afisa
Mifugo wa Kata ya Salawe, Gasper Ronald Makawa, ambaye amempongeza mwandaaji wa
ligi hiyo Bwana Makamba Lamecki, kwa juhudi zake za kuibua na kuendeleza vipaji
vya vijana na kwamba amewasihi wachezaji kutumia mashindano hayo kama fursa ya
kufikia ndoto zao katika michezo.
Viongozi wengine waliotoa pongezi ni Mwenyekiti wa
Kijiji cha Songambele, Lazaro Enock Lazaro, Mtendaji wa Kijiji cha Songambele,
Evalina Isack, na Afisa Maendeleo wa Kata ya Salawe Emmy Kwayu pamoja na mambo
mengine wamesema ligi hiyo ni msaada mkubwa kwa vijana na ni tukio linaloleta
mshikamano miongoni mwa wananchi, hasa kwa kuwa mashindano hayo ni bure kwa
wananchi wote.
Msimamizi wa Ligi ya Krismas Cup, Mwalimu Emmanuel
Enock Kijida, ametoa taarifa ya mechi inayofuata.
"Kesho kutakuwa na mechi kati ya Salawe
FC na Solwa FC, kwa hiyo atakayeshinda mechi ya kesho ndiye atakayekutana na
mshindi wa mechi ya leo, ambaye ni Mwabenda FC. Nawakaribisha sana wananchi
wote kuja kuburudika, kwani hii mechi ni ya derby." Amesema Mwalimu Kijida
Mashindano haya yanatarajiwa kufikia kilele tarehe
17 Disemba 2024, kwa fainali itakayofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi
Mhangu, Kijiji cha Songambele ambapo Mfumo wa mtoano utaendelea kutumika hadi
hatua ya mwisho.
Ligi hii, iliyoandaliwa na Makamba Mussa Lameck
kupitia kampuni yake ya MCL inayojihusisha na biashara ya nafaka, imelenga
kuibua vipaji vya michezo katika Mkoa wa Shinyanga huku ikileta mshikamano wa
kijamii.
Kwa habari zaidi kuhusu mashindano haya na matukio mengine ya michezo, endelea kufuatilia MISALABA MEDIA.
Mgeni rasmi wa mechi ya leo Disemba 1, 2024 ni Afisa
Mifugo wa Kata ya Salawe, Gasper Ronald Makawa, akimpongeza Makamba Lameck kwa
kuandaa ligi ya michezo bila wananchi kutoa hela.
Mgeni rasmi wa mechi ya leo Disemba 1, 2024 ni Afisa
Mifugo wa Kata ya Salawe, Gasper Ronald Makawa, akimpongeza Makamba Lameck kwa
kuandaa ligi ya michezo bila wananchi kutoa hela.
Msimamizi wa Ligi ya Krismas Cup, Mwalimu
Emmanuel Enock Kijida, akitoa taarifa ya mechi inayofuata.
Post a Comment