" BABA NA MTOTO KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUKUTWA NA BANGI KILO 398

BABA NA MTOTO KIFUNGO CHA MAISHA KWA KUKUTWA NA BANGI KILO 398

Na Lucas Raphael, Misalaba Media -Tabora
 
Mahakama ya hakimu mkazi wilaya ya nzega mkoani tabora  imewahukumu kifungo cha maisha jela baba na mtoto kwa kukutwa na hatia ya kusafirisha bangi kutoka nzega Tabora na kuzipileka mkoani shinyanga kinyeme na sheria za nchi.
 
Familia hiyo ilitiwa hatiani  jana na  hakimu mkazi mwandamizi wilaya ya nzega mkoani hapa ,Saturini Mushi baada ya  kuona washitakiwa kuwa na kosa na hujumu uchumi .
 
Mushi aliwataja waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kuwa ni familia moja ambayo ni  baba aliyetambulika kwa jina  Ally Thabit  (45)na mtoto Jonas Ally Thabiti (23) alisema kwa kifungo hicho kiwe fundisho kwa watu wengine wanaofanya  biashara ya madawa ya kulevya yaliyokatazwa kutokana na sheria za Tanzania.
 
Hakimu huyo alibainisha kwamba hukumu hiyo itakuwa ni mwanzo wa kukomesha vitendo vya kiulihalifu kwa wananchi kulima na kuunza bangi kinyume na sheria za Jamhuri ya muungano wa Tanzania .
 
Awali Mwendesha Mashitaka kutoka mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Meshaki Lyabonge aliiambia mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi ya wilaya ya nzega mkonai Tabora kwamba mnamo machi 13 mwaka jana  katika msitu wa Mabatini, kijiji cha Kigandu kata ya Mogwa wilayani humo watu hao  wakiwa na pikipiki walikamatwa wakisafirisha bangi kwenye magunia wakipeleka mkoani Shinyanga 
 
Mwendesha mashitaka huyo aliomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iliwe fundisho kwa walimaji wengine wa mazao ya aina hiyo nchini na kutaja kesi namba ya 7152 ya mwaka 2024.
 
 Aidha washitakiwa hao waliomba kupunguziwa adhamu waliiambia Mahakama hiyo kwamba hilo ni kosa lao la kwanza hivyo wanaomba mahakama iwasemehe kwani hatarudia tena.
 
Hata hivyo hakimu hiyo alitupilia mbali ombi hilo na kutamka kifungo cha maisha jela na kupatiwa muda wa kakata rufaa kama hawakuridhika na  hukumu hiyo.
 
mwisho 

Na Lucas Raphael,Tabora
 
Post a Comment

Previous Post Next Post