Na Mapuli Kitina Misalaba
Bonanza la michezo mbalimbali linalojulikana kwa jina la Malula Home Talents Competition limefunguliwa rasmi katika uwanja wa shule ya msingi Kitangili, Manispaa ya Shinyanga, likiwa na lengo la kukuza vipaji na kuhamasisha maendeleo ya kijamii kupitia michezo.
Akifungua rasmi bonanza hilo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Afisa Tarafa wa Wilaya hiyo Telezia Kalunga Alois, amempongeza mratibu wa bonanza hilo Daniesa Malula kwa kubuni wazo lenye tija kwa jamii, akisema kuwa linachangia kuinua vipaji na kutoa ajira kupitia michezo.
“Niwatake vijana kutumia fursa hii kujiendeleza na vipaji vyao badala ya kujiingiza kwenye makundi mabaya kama vile ya uvutaji wa sigara na matumizi ya madawa ya kulevya,” amesema Kalunga.
Amesisitiza pia umuhimu wa kudumisha amani kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, huku akihimiza ushiriki wa wananchi wote katika zoezi hilo la kidemokrasia.
Katika bonanza hilo, michezo mbalimbali inafanyika ikiwemo:
-
💥 Home Marathon
-
⚽ Mpira wa miguu (Timu 6)
-
🚲 Mbio za baskeli
-
🍽️ Mashindano ya kula
-
💪 Mashindano ya kuvuta kamba
-
💃 Mashindano ya dance
-
🏍️ Mashindano ya pikipiki
-
🎶 Burudani ya ngoma za utamaduni na jadi kutoka Wilaya ya Shinyanga
Kwa upande wa mpira wa miguu, baadhi ya mechi zinazopigwa ni kati ya Station FC dhidi ya Migos FC, Busulwa FC dhidi ya Bodaboda FC na Brack Tiger U20 dhidi ya Busulwa U20.
Bonanza hili linaendelea katika viwanja hivyo vya Kitangili na linatarajiwa kufungwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Wakili Julius Mtatiro.
Post a Comment