" DKT. HAJI MNASI: KIONGOZI MAHIRI NA MZALENDO WA KWELI

DKT. HAJI MNASI: KIONGOZI MAHIRI NA MZALENDO WA KWELI

Katika tasnia ya uongozi wa umma, mara chache sana hupatikana viongozi wenye sifa za kipekee, maono ya mbali na moyo wa kujitolea kama Dkt. Haji Mnasi. Akiwa ni mzawa wa Wilaya ya Newala, Dkt. Mnasi amejipambanua kama kiongozi mwenye dira, anayewatumikia wananchi kwa uadilifu, ufanisi na weledi wa hali ya juu. Kwa sasa akiwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Dkt. Mnasi ameendelea kudhihirisha kuwa uongozi bora hauhitaji kelele bali matendo yenye tija kwa jamii.


Kabla ya kupewa dhamana ya kuiongoza Siha, Dkt. Mnasi alihudumu kwa miaka mitano kama Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje ambapo alianzisha mageuzi makubwa katika sekta mbalimbali kama elimu, afya, kilimo na miundombinu. Pia aliwahi kushikilia nafasi ya Mkuu wa Idara ya Elimu katika Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), na katika Halmashauri mbalimbali kama Ludewa, Iringa na Mtwara. Katika kila eneo alilopangiwa kazi, Dkt. Mnasi alionyesha umahiri, kujituma, na kuacha alama isiyofutika katika maendeleo ya jamii.


Moja ya maeneo ambayo Dkt. Mnasi ameonyesha umahiri mkubwa ni katika sekta ya elimu. Kupitia nafasi zake za uongozi, amesimamia na kuhimiza utoaji wa elimu bora, ujenzi wa miundombinu ya shule, na upatikanaji wa vifaa vya kujifunzia. Aidha, juhudi zake zimekuwa zikiwalenga pia watoto, ambapo amekuwa mstari wa mbele kupambana na changamoto za malezi na maadili katika kizazi cha sasa. Kwa kulitambua hili, mwaka 2025 Dkt. Mnasi alizindua kitabu chake kilichopewa jina la “Elimu na Malezi ya Watoto Katika Zama za Kidijitali”. Kitabu hiki ni hazina muhimu ya maarifa na mbinu mbalimbali za kuwasaidia wazazi, walimu na walezi katika kulea watoto wanaokua katika mazingira ya teknolojia ya kisasa.


Uongozi wa Dkt. Haji Mnasi umejengwa juu ya misingi ya maadili, uwazi na uwajibikaji. Ni kiongozi mwenye maono ya mbali na anayefanya maamuzi kwa busara, akizingatia maslahi ya wengi. Amejenga mazingira mazuri ya kazi kwa watumishi wa umma, kuimarisha uwajibikaji na kushirikisha jamii katika shughuli za maendeleo. Hakika, utendaji wake umekuwa mfano kwa viongozi wengine nchini na ushuhuda wa kuwa uongozi bora huenda sambamba na kujifunza kila siku.


Dkt. Mnasi si tu kiongozi, bali ni taasisi. Anaifahamu jamii, anaijali, na anaweka mbele maslahi ya wananchi. Elimu yake ya PhD imemuwezesha kuchanganya maarifa ya kitaaluma na uzoefu wa vitendo, na hivyo kuwa kiongozi anayehitajika katika zama hizi za mabadiliko ya kijamii na kiteknolojia. Kwa mchango wake mkubwa katika maeneo mbalimbali, Dkt. Mnasi ameacha historia ya heshima, siyo tu katika maeneo aliyohudumu, bali kwa Taifa zima la Tanzania.


Post a Comment

Previous Post Next Post