" Gwajima Azidi Kukichachafya Licha Kukosolewa na Wabunge Wenzake

Gwajima Azidi Kukichachafya Licha Kukosolewa na Wabunge Wenzake

 

Gwajima Azidi Kukichachafya Licha Kukosolewa na Wabunge Wenzake

Moja kati ya kiongozi wa kisiasa ambaye amezua gumzo mtaani lakini pia katika vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla wiki hii ni Askofu Josephat Gwajima. Mbunge wa jimbo la Kawe ambaye aliongea siku chache zilizopita kuhusu utekaji.

Mbali na maneno yake kuhusu utekaji kuchukua taswila mbaya kwa kukosolewa na viongozi wengi wa siasa nchini Tanzania ikiwemo wabunge wenzake, Gwajima ameona isiwe tabu na kugeukia upande wapili kuongelea maono ya nchi na maendeleo katika taifa la Tanzania kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika ukurasa huo maalum wa Askofu Josephat Gwajima, aliposti video yake akiwa Bungeni. Katika video hiyo alisikika akisema juu ya maendeleo ya Tanzania ambapo alitoa ushauli wake ule ule anaoutoa kila siku kuhusu maono ya muda mrefu katika nchi.

Gwajima alidai kuwa, taifa linatakiwa kuwa na maono ya nchi na kukili kuwa kama kila Rais atakuwa na mipango yake basi taifa litaendelea kuyumba kila kukicha kwasababu hakuna msimamo kamili wa nchi. Lakini kwa upande wake alidai kuwa inatakiwa kuwe na malengo ya miaka 50, ambayo kila Rais atafuata malengo hayo, huku akisisitiza kuwa hata wananchi watajua kipaumbele cha taifa lao.

Post a Comment

Previous Post Next Post