" WADAU WA MICHEZO NA WANANCHI WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUANGALIA VIPAJI VYA VIJANA KATIKA LIGI YA NIACHEKONA

WADAU WA MICHEZO NA WANANCHI WAHAMASISHWA KUJITOKEZA KUANGALIA VIPAJI VYA VIJANA KATIKA LIGI YA NIACHEKONA

Na Mapuli Kitina Misalaba

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea katika uwanja wa Mwabenda kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga yameendelea kushika kasi ambapo timu ya KIMANDAGULI FC (KUNGULU WEUSI) imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KASHISHI FC katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na kuvutia mashabiki wengi waliojitokeza kushuhudia burudani ya soka.

Baada ya mchezo huo, Katibu wa Kamati ya Mashindano Sambayi Jilya ametangaza ratiba ya mechi zinazofuata huku akiendelea kuwakumbusha wananchi wa jimbo la Solwa pamoja na maeneo jirani kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda kushuhudia michezo hiyo inayozidi kuleta burudani na kuibua vipaji vya vijana.

Amesema mechi ya kesho ni timu ya ISENENGEJA itamenyana na MWAKITOLYO No.6 katika pambano linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja wa Mwabenda.

Amesema mashindano hayo yanaendelea kuwa jukwaa muhimu la kukuza michezo pamoja na kuimarisha mshikamano wa jamii kupitia soka.

Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Bwana Paul Daud Augustino kupitia ufadhili wa Lushu Foundation kwa lengo la kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo pamoja na kuhamasisha mshikamano miongoni mwa wananchi.

Kwa huduma za ushereheshaji wa shughuli mbalimbali, matangazo pamoja na burudani unaweza kuwasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

Timu ya Kashishi FC


 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post