" HAWA SIRI AWAHIMIZA MAKADA WA CCM KATAVI KUIMARISHA UMOJA NA UWAJIBIKAJI

HAWA SIRI AWAHIMIZA MAKADA WA CCM KATAVI KUIMARISHA UMOJA NA UWAJIBIKAJI


Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndg. Hawa Siri Makonyola, akiwa katika kikao cha pamoja na Makada wa CCM Mkoa wa Katavi, kilichofanyika leo tarehe 05/10/2026 katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda.

Kaimu Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Katavi, Ndg. Hawa Siri Makonyola, amewahimiza Makada wa CCM mkoani humo kuimarisha umoja, mshikamano na uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya chama, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi katika uingizaji wa wanachama wapya na ulipaji wa ada za uanachama.

Hawa Siri ametoa kauli hiyo  Oktoba 5, 2026, wakati akizungumza katika kikao cha pamoja na Makada wa CCM Mkoa wa Katavi, Sekretarieti za Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpanda pamoja na wajumbe wa Kamati za Siasa za Mkoa na Wilaya.

Amesema kikao hicho kililenga kuwapa nafasi viongozi na Makada hao kufahamiana, kusalimiana na kutambuana, pamoja na kupokea maelekezo mbalimbali ya chama yatakayosaidia kuimarisha utendaji na utekelezaji wa majukumu ya CCM katika Mkoa wa Katavi.

Katika kikao hicho, Hawa Siri amesisitiza umuhimu wa kuwa na upendo na amani miongoni mwa viongozi na wanachama, akieleza kuwa hali hiyo ni muhimu katika kujenga mazingira mazuri ya kufanya kazi pamoja na kuongeza hamasa ya wanachama katika kutekeleza majukumu yao.

Aidha, amewataka Makada hao kuzingatia maadili mema katika uongozi, ikiwa ni pamoja na uaminifu, utulivu, uvumilivu, uzalendo, upendo, uadilifu na nidhamu, huku akiwataka kutekeleza majukumu yao kwa nguvu, ufanisi na weledi kwa kuzingatia maelekezo na taratibu za chama.

Hawa Siri pia amesisitiza suala la uwajibikaji, akiwataka Makada kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatekeleza majukumu waliyopewa kwa wakati, pamoja na kuendelea kuhamasisha wananchi kujiunga na CCM na wanachama kutimiza wajibu wao wa kulipa ada, akieleza kuwa hatua hiyo ni miongoni mwa misingi ya kuimarisha uhai wa chama na jumuiya zake.

Katika hatua nyingine, kikao hicho kimejadili umuhimu wa kuendelea kutoa mafunzo kwa viongozi na wanachama katika Kata mbalimbali za Mkoa wa Katavi, kwa lengo la kuwawezesha kufahamu zaidi Chama Cha Mapinduzi, misingi yake, taratibu na namna ya kutekeleza majukumu ya chama kwa ufanisi.

Kikao hicho kimewakutanisha Makada wa CCM pamoja na Sekretarieti za Mkoa wa Katavi na Wilaya ya Mpanda, huku kikilenga kuimarisha ushirikiano na utendaji wa pamoja katika utekelezaji wa majukumu ya chama mkoani humo.

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndg. Hawa Siri Makonyola, Oktoba 5, 2026, amefanya kikao kazi na Makada wa CCM Mkoa wa Katavi katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda.

Kaimu Katibu wa CCM Mkoa wa Katavi, Ndg. Hawa Siri Makonyola,  tarehe 05/10/2026 akiendelea kutoa maelekezo mbalimbali kwa Makada wa CCM Mkoa wa Katavi katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda, hususan kwa Makada waliopata mafunzo ya kiuongozi Zanzibar.Ndg. Fortunata Kabeja, Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Katavi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Katavi,  tarehe 05/10/2026 ameshiriki kikamilifu katika kikao cha pamoja na Makada wa CCM Mkoa wa Katavi kilichofanyika katika Ukumbi wa CCM Wilaya ya Mpanda. Katika kikao hicho, amehimiza umuhimu wa kuingiza wanachama wapya pamoja na kuwakumbusha wanachama kutekeleza wajibu wao wa kulipa ada ya uanachama.


Post a Comment

Previous Post Next Post