Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Mbeya
Shule ya Awali na Msingi ya Mbeya Bright Stars, iliyopo Kata ya Iwambi, Mtaa wa Lumbila mkoani Mbeya, imeanza rasmi mchakato wa kutoa fomu za usajili wa wanafunzi wapya kwa ajili ya mwaka wa masomo wa 2027.
Usajili huo unahusisha wanafunzi wanaojiunga na madarasa ya awali, darasa la kwanza, pamoja na wanaohamia.
Akizungumza na Misalaba Media, Oktoba 02, 2026, Mkuu wa Shule hiyo, Mwalimu Salome Isack, amewahimiza wazazi na walezi kuwapeleka watoto wao katika shule hiyo, akisisitiza kuwa inatoa elimu bora katika mazingira salama, ya kuaminika na yenye kuwajenga vyema watoto.
Mwalimu Salome ameeleza kuwa masomo na huduma zinazotolewa shuleni hapo zimepangwa kimkakati kuendana na Dira ya Maendeleo ya Taifa (2025–2050)—mpango wa muda mrefu wa Serikali unaolenga kuifanya Tanzania kuwa Nchi yenye uchumi imara, utawala bora, maisha bora kwa Wananchi, na jamii yenye elimu na afya bora hivyo kupitia misingi hiyo, Mbeya Bright Stars inajikita katika kujenga rasilimaliwatu itakayofikia malengo hayo ya kitaifa.
Mwalimu huyo amewasihi wazazi kuwekeza zaidi kwenye malezi ya mtoto na si matunzo pekee .
Amesema kuwa ili kupata mtoto mwenye heshima na nidhamu, ushirikiano katika malezi ni jambo la muhimu kwani Tanzania ya kesho itajengwa na watoto waliolelewa vyema, hivyo kazi hii isiwe ya walimu au Serikali pekee, bali ni ya wazazi na walezi wote," amesisitiza Mwalimu Salome.
Mbeya Bright Stars ni shule ya kutwa na jumuishi inayopokea pia watoto wenye mahitaji maalum na inatoa huduma na fursa mbalimbali, ikiwemo:
Usafiri wa Uhakika, kwa wanafunzi wanaotoka mbali,
Elimu ya kisasa na Stadi, Elimu ya kompyuta, michezo, elimu ya dini, na stadi za karne ya 21.
Ameongeza kuwa ulinzi na usalama wa mtoto upo wa kutosha ambapo kuna uzio thabiti, mfumo wa kamera za usalama (CCTV), na daftari maalum la usajili wakati wa kuingia na kuondoka ili kuhakikisha mtoto anakabidhiwa mikononi mwa mzazi au mlezi wake salama.
Pia ameongeza kuwa shule hiyo imejidhatiti hasa katika masuala ya Afya na lishe bora ambapo watoto hupata Kifungua kinywa na chakula cha mchana vinavyozingatia makundi yote sita ya chakula, matunda, na mboga mboga, huku watoto wadogo wakiongezewa milo ya ziada.
Aidha amesema kuwa shule hiyo inashirikiana na idara ya Afya katika kampeni za kutoa chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na dawa za minyoo, ikisaidiwa na chumba cha huduma ya kwanza na upatikanaji wa maji safi na salama.
Mwalimu Salome ameishukuru Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wanawake kuwekeza katika elimu na biashara.
Ametoa shukrani za dhati kwa Idara ya Elimu, Idara ya Udhibiti ubora wa Elimu, waratibu Elimu, na taasisi za Kifedha zilizotoa ushirikiano na mikopo iliyowezesha uboreshaji wa shule hiyo.
Hata hivyo Mwalimu Salome amebainisha kuwa madhamira kuu ya Mbeya Bright Stars ni kuendelea kuwekeza kwenye teknolojia ya kisasa na miundombinu ya kidijitali ambapo hatua hiyo haitaimarisha tu ufaulu wa kiwango cha juu darasani, bali pia itaipeperusha shule hiyo kuwa kinara na kielelezo cha elimu bora mkoani Mbeya na taifa kwa ujumla.
PROFESSOR MGOKO EPISODE 04
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment