Na Lucaas Raphael,Tabora
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wananchi wa mkoa wa Tabora kujitokea katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kwenye vituo walivyojiandikishia na kutazama daftari la awali lilolowekwa wazi na kutoa taarifa za wale waliokosa sifa kuwepo kwenye daftari hilo
Akizungumza baada ya kutembelea vituo katika Halmashauri za Manispaa ya Tabora Mkurugenzi wa Tume Huru ya Uchaguzi - INEC, Ramadhan Kailima alisema wananchi wameonesha mwitikio wakati wa zoezi hili wamejitokeza kuwataka kuhakiki taarifa zao.
Alisema kwamba Tume imeweka wazi daftari la awali la wapiga kura katika vituo vyote vilivyotumika kuandikisha na kuboresha taarifa za Wapiga kura katika awamu ya pili hivyo wananchi wajitokeze kuhakiki taarifa zao na kutoa taarifa za wale ambao hawastahili kuwepo katika Daftari hilo.
“Nawasihi wananchi endapo wataona katika Daftari ambalo tumeliweka katika kila kituo kuna mwananchi ambaye amekosa sifa kama vile kufariki basi wawe huru kwa kutumia fomu namba 5B kumuondoa huyo ambaye amekosa sifa za kuwepo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura.”alisema.
Aidha, alisema kwamba mkoa wa Tabora unavituo vya kujiandikishia daftari la mpiga kura vipo 376 mkoa mzima .
Hata hivyo alisisitiza wananchi waendelee kujitokeza katika kuboresha taarifa zao wale ambao hawakuboresha taarifa zao katika awamu ya kwanza ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura basi ndio kipindi cha kafanya hivyo.
Aidha tume inatoa nafasi kwa watu wote wenye changamoto ya kutoa kuona kusikia na kutoajua kusioma wanatakiwa kuja na watu wao wenye uwezo wa kuwasaidia ili waeze kujiandikasha kwenye Daftari la mpiga kura .
Naye mratibu wa uhamasishaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoawa Tabora Heri Huruma Nyela alisema kwamba hali ya uandisha katika mkoa wa Tabora enendelea vizuri na watu wanajitokea vizuri
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili unafanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kuanzia Mei 01, 2025 na kukamilika tarehe 07 mikoani hapa .
Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza utajumuisha mikoa 15, mzunguko wa pili mikao 16 pomoja na vituo vya magereza na vyuo vya mafunzo.
mwisho
Post a Comment