Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza
na Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati
alipotembelea mafunzo ya siku moja ya watendaji hao ambayo yanahusisha waandikishaji
wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kutoka Kata zote za Halmashauri ya
Mji wa Kibaha mkoani Pwani. Zoezi la uboreshaji awamu ya pili linataraji kuanza
Mei 16 hadi 22, 2025 sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la Wapiga
Kura na vituo vitafunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.

Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele akizungumza
na Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura wakati
alipotembelea mafunzo ya siku moja ya watendaji hao ambayo yanahusisha waandikishaji
wasaidizi na waendesha vifaa vya bayometriki kutoka Kata zote za Halmashauri ya
Mji wa Kibaha mkoani Pwani. Zoezi la uboreshaji awamu ya pili linataraji kuanza
Mei 16 hadi 22, 2025 sambamba na uwekaji wazi wa daftari la awali la Wapiga
Kura na vituo vitafunguliwa kuanzia Saa 2:00 asubuhi hadi Saa 12:00 jioni.
Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Hidaya Gwandu akizungumza

Mapema kabla ya kuanza kikao hicho Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele leo Mei
14, 2025 amemtembelea na kufanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhe.
Abubakar Kunenge ofisini kwake. Mwenyekiti wa Tume na ujumbe wake wapo mkoa wa
Pwani kwaajili ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
ambalo linaingia awamu ya pili katika mikoa 16 ya Tanzania Bara na Zanzibar
ukiwepo mkoa wa Pwani pamoja na uwekaji wazi wa Daftari la awali la wapiga
kura. ************************
Na Mwandishi wetu, Pwani
TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi imewataka wananchi
kutoka mikoa 16 ya Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar wanaokwenda kuanza
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu yapili kujitokeza
kuboresha taarifa zao pamoja na kutazama daftari la awali la Wapiga Kura lililobandikwa
katika vituo walivyotumia kujiandikisha au kuboresha taarifa zao hap[o awali.
Hayo yamesemwa leo Mei 14, 2025 na Mwenyekiti
wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufaa Jacobs Mwambegele wakati akizungumza
na washiriki wa mafunzo ya siku moja ya watendaji wa Uboreshaji kutroka
Halmashauri ya Mji wa Kibaha Mkoani Pwani.
“Niwasisitize watanzania wote katika mikoa
hii 16, wajitokeze kuja kuboresha taarifa zao au kuja kujiandikisha kwasababu
baada ya hapa Tume haita boresha tena Daftari…litaboreshwa kuanzia tarehe 16
hadi 22 Mei kwa muda wa siku saba,”alisema Jaji Mwambegele.
Aidha, mzunguko wa pili utahusisha mikoa ya
Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Morogoro, Pwani, Singida, Dodoma, Dar es
Salaam, Lindi, Mtwara, Mjini Magharibi, Kaskazini Unguja, Kusini Unguja,
Kaskazini Pemba na Kusini Pemba ambapo zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 16
hadi 22, 2025.
Katika hatua nyingine Jaji Mwambegele
amewakumbusha watendaji hao wa uboreshaji ambao ni Waandikishaji Wasaidizi na
waendesha vifaa vya Biometriki kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na
taratibu za Uchaguzi wakati wa utekelezaji wa awamu ya pili ya zoezi hilo litakalofanyika
sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura.
“Nawakumbusha tena kama nilivyowakumbusha
katika zoezi lililopita, kwamba katika utekelezaji wa zoezi hili mzingatie
sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi, muwe wanyenyekevu kwa wateja mtakao
kuwa mnawahudumia,”alisema Jaji Mwambegele.
“Zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa
masharti ya kifungu cha 16(5) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na
Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024 kinachoipa Tume jukumu la kuboresha Daftari la
Kudumu la Wapiga Kura mara mbili mara baada ya uchaguzi mkuu na kabla ya uteuzi
wa wagombea kwa uchaguzi mkuu unaofuata.
Nae Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya Mji
wa Kibaha, Dkt. Rogers Shemwelekwa amewataka wananchi wa Kibaha na viunga vyake
kujitokeza kutazama daftari la awali lililowekwa wazi na kama kuna changamoto
waweze kuziboresha wakati huu.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura awamu ya pili ulianza kufanyika sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la
Awali la Wapiga Kura kuanzia tarehe 01 Mei, 2025 na kukamilika tarehe 04 Julai,
2025.
Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa
mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza ulihusisha mikoa 15, mzunguko wa
pili mikoa 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na vyuo vya
mafunzo.
Mikoa iliyohusika kwenye mzunguko wa kwanza
wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza,
Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo
zoezi hilo litafanyika kuanzia Mei 1 hadi 7 mwaka huu.
Mzunguko wa tatu wa zoezi la uboreshaji wa
Daftari utahusisha vituo 130 vilivyopo kwenye magereza ya Tanzania Bara na
vituo 10 vilivyopo katika Vyuo vya Mafunzo Tanzania Zanzibar kwa wakati mmoja
na utafanyika kwa muda wa siku saba kuanzia Juni 28 hadi Julai 04, 2025.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura kwa awamu ya pili, utafanyika ngazi ya kata kwa Tanzania Bara na ngazi ya
jimbo kwa Tanzania Zanzibar, ambapo jumla ya vituo 7,869 vitahusika, vituo
7,659 vipo Tanzania Bara na vituo 210 vipo Tanzania Zanzibar.
Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga
kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa
zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za
kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
Mambo mengine ni kuhamisha taarifa za wapiga
kura waliohama kutoka kata au jimbo walipoandikishwa awali na kuondoa taarifa za wapiga kura waliopoteza sifa za
kuwemo kwenye Daftari kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kifo.
Aidha, kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha
11(1) na (2) cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya Mwaka
2024, Tume pia ina jukumu la kuandaa Daftari la Awali la Wapiga Kura na
kuliweka wazi kwa umma.
Lengo la uwekaji wazi wa Daftari hilo ni kutoa
fursa kwa wananchi kukagua, kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura na
uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga kura waliomo kwenye daftari ambao hawana
sifa na litabandikwa katika vituo vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya kwanza.
Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25
Machi, 2025.Baadhi ya viongozi wa Halmashauri wanaoshughulika na Uboreshaji huo wakiwa katika mafunzo. 
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia nasaha za Mwenyekiti wa Tume wakati akizungumza.
Post a Comment