Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (kulia) akikagua mwenenedo wa uboreshaji Daftari katika Halamashauri ya Songea Vijijini.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (shati la drafti) akiwa katika kituo cha shule ya Msingi Mahela katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkoa huo jana. Kulia walio simama ni Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Mbinga Mjini, Ndg. Amina Hamisi Seif. (Picha na INEC).
Wananchi wakiangalia Daftari la awali la wapiga kura lililowekwa wazi.
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (kulia) akiwa katika kituo cha shule ya Msingi Mahela katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga Mkoani Ruvuma wakati akitembelea vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mkoa huo jana. Wapili Kulia ni Afisa Mwandikishaji wa Jimbo la Nyasa, Ndg. Khalid Khalifa. (Picha na INEC).
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele (Kushoto) akimkabidhi kadi ya Mpiga Kura Ndg. Acheni Maulid mkazi wa Mbamba Bay katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasamkoani Ruvuma aliyefika katika kituo cha Shule ya msingi Mbamba bay kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. (Picha na INEC).
Mpiga Kura Ndg. Acheni Maulid mkazi wa Mbamba Bay katika Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma akionesha aliyefika katika kituo cha Shule ya msingi Mbamba bay kuboresha taarifa zake katika Daftari la Kudumu la Mpiga Kura. (Picha na INEC).
Na Mwandishi Wetu, Ruvuma
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imewataka wananchi wa mikoa 15 inayotekeleza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika mzunguko wa kwanza wa awamu ya pili kuzitumia siku chache zilizobaki katika mikoa yao kuhakikisha wanajitokeza kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao ili wasijekosa haki yao ya msingi ya kupiga Kura katika uchaguzi ujao mwaka huu.
Hayo yamesema na Mwenyekiti wa Tume Huru ya
Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele wakati akitembelea
vituo mbalimbali vya uboreshaji wa Daftari hilo katika Katika halsmahauri za
Mkoa wa Ruvuma.
“Nawasihi wananchi wa mikoa 15 ambayo awamu
ya pili ya Uboreshaji Daftari inafanyika wandelee kujitokeza kuja kuboresha,
waendelee kujiandikisha lakini pia kuwaondoa wale ambao hawastahili kuwa katika
Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, tumebakiwa na siku chache zinazotakiwa
kuendelea na zoezi,” alisema Jaji Mwambegele.
Jaji Mwambegele amesema zoezi la uboreshaji
wa wa awamu ya pili linakwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la awali la
kudumu la wapiga Kura ambalo linatoa fursa kwa wananchi kukagua, kufanya
marekebisho ya taarifa za wapiga kura na uwekaji wa pingamizi dhidi ya wapiga
kura waliomo kwenye daftari ambao hawana sifa na litabandikwa katika vituo
vyote vilivyotumika wakati wa uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura
awamu ya kwanza.
Akizungumzia kuhusu mwenendo wa zoezi hilo
kwa ujumla Jaji Mwambegele amesema zoezi linakwenda vizuri na mwitikio wa
wananchi ni mzuri kwani maeneo aliyotembelea katika mikoa ya Iringa, Njombe na
Ruvuma wananchi wamejitokeza vituoni kujiandikisha, kuboresha taarifa zao pamoja
na kutoa taarifa za watu waliopoteza sifa za kuwepo kwenye Daftari hilo.
“Kwa ujumla wake zoezi linakwenda vizuri na
wananchi wengi wamejitokeza kwaajili ya kuboresha taarifa zao, wamejitokeza pia
kwaajili ya kuboresha taarifa zao na pia, wale ambao hawastahili kuwepo katika
Daftari la Kudumu la Wapiga kura wamefutwa,katika kila kituo nil;ichokwenda
wameniambia kuhusu wale walio waandikisha, waboresha na wale waliowafuta,”
alisema.
Uboreshaji wa Daftari unafanyika kwa
mizunguko mitatu ambapo mzunguko wa kwanza unajumuisha mikoa 15, mzunguko wa
pili utajumuisha mikoa 16 na mzunguko wa tatu utajumuisha vituo vya magereza na
vyuo vya mafunzo.
Mikoa inayohusika kwenye mzunguko wa kwanza
wa uboreshaji ni pamoja na Iringa, Geita, Kagera, Mara, Shinyanga, Mwanza,
Simiyu, Rukwa, Tabora, Katavi, Kigoma, Ruvuma, Mbeya, Njombe na Songwe ambapo
zoezi hilo lilianza kutekelezwa tangu Mei 1 na linataraji kukamilika Mei 7
mwaka huu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Maafisa
Waandikishaji kutoka Majimbo ya Nyasa, Ndg. Khalid Khalifa na yule wa Jimbo la
Mbinga Mjini Ndg. Amina Hamisi Seif wamesema zoezi la Uboreshaji katika maeneo
yao linakwenda vizuri na kuwahimiza wananchi kuendelea kujitokeza.
“Kwa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa
tumekwisha andikisha wapiga kura wapya 436 na kuboresha taarifa za wapiga kura
415 wakati wapiga kura 68 wamepoteza sifa na kufutwa katika Daftari la Kudumu,
bado tuzazo siku hivyo niombe kutumia fursa hii kuwataka wananchi waendelee
kujitokeza,” alisema Khalifa.
Katika awamu ya pili ya uboreshaji, wapiga
kura wapya 1,396,609 wataandikishwa, wapiga kura 1,092,383 wataboresha taarifa
zao na wapiga kura 148,624 watafutwa kwenye Daftari kwa kukosa sifa za
kuendelea kuwepo kwenye Daftari,” amesema Jaji Mwambegele.
Tume iliboresha Daftari la Kudumu la Wapiga
Kura awamu ya kwanza kuanzia tarehe 20 Julai, 2024 na kukamilisha tarehe 25
Machi, 2025.

Post a Comment