Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima, akiwasaidia wananchi kuhakiki majina yao kabla ya kwenda kuboresha taarifa zao katika Kituo cha kuandikisha wapiga kura, Ofisi ya Kata ya Isevya, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, wakati alipotembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura Mkoani Tabora, leo Mei 04, 2025. Picha na INEC
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima, akimkabidhi kadi ya mpiga kura Mwanafunzi wa Kidato cha Sita wa Shule ya Sekondari ya Milambo, Maboto Wambura, wakati alipokitembelea Kituo cha Kuandikisha Wapiga Kura katika shule hiyo iliyopo Kata ya Chemchem, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, Mei 4, 2025. Picha na INEC
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima, akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana Tabora, wakati alipotembelea Kituo cha Kujiandikisha Wapiga Kura kilichopo shuleni humo, Mei 04, 2025, ambapo pia aliwahamasisha wanafunzi wa shule hiyo na Sekondari ya Milambo zilizopo katika Hamlashauri ya Manispaa ya Tabora, wajitokeze kujiandikikisha kwa walio na sifa. Picha na INEC.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg. Ramadhani Kailima (kulia), akizungumza na mwendesha kifaa cha ‘Bayometriki’ katika Kituo cha kuandikisha wapiga kura kilichopo Kata ya Isevya, Halmashauri ya Manispaa ya Tabora, alipotembelea na kukagua vituo vya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura awamu ya pili linalokwenda sambamba na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura Mkoani Tabora, leo Mei 04, 2025. Katikati ni Mratibu wa Uandikishaji Mkoa wa Tabora, Elihuruma Nyella. Picha na INEC

***************
Na Mwandishi Wetu, Tabora.MKURUGENZI wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Ndg Ramadhani Kailima amewataka wananchi wa Mkoa wa Tabora kujitokeza kuhakiki na kuboresha taarifa zao katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na uwekaji wazi wa Daftari la Awali la Wapiga Kura kwenye vituo walivyojiandikishia na kutazama daftari la awali lilolowekwa wazi na kutoa taarifa za wale waliokosa sifa kuwepo kwenye daftari hilo
Post a Comment