
Mbunge Acharuka: Watoto Wetu Wanakata Viuno Kama Feni Mashuleni, Sio Sawa
Mbunge wa Viti Maalumu Tauhida Cassian Gallos amemtaka Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu kutoa zuio na kalipio kwa shule zinazowafundisha watoto wa shule za awali na msingi kucheza (kukata viuno) kwenye sherehe za mahali.
Tauhida ametoa kauli hiyo wakati akichangia mjadara wa makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwka wa fedha 2025/26 ambapo amesema kitendo hicho noi kinyume na maadili na kinaweza kuharibu Watoto.
“Nimesimama kwa masikitiko makubwa Watoto wale sasahivi kwenye mahafali zao kutoka shule za nursery Kwenda Primary wanafungwa kanga za kiuno na tena wanafungwa kanga mbili Waziri toa tamko tena tamko kali si kwa walimu si kwa shule najua kuna wizara ya Elimu lakini suala la malezi ni la wizara yako tena watoto wa kike akishafungwa hiyo Kamba kiunoni na macho anapeleka juu anakata kiuno neti ni kiasi lakini haitoshi kuna Watoto wetu wa kiume wanakata viuno mpaka unafika wakati unasema imekuwaje” Tauhida Cassian Gallos – Mbunge wa Viti Maalum
Post a Comment