
Mrithi wa Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi anatarajiwa kupatikana muda wowote ndani ya saa 24 katika Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi unaoanza leo Mei 29,2025 jijini Dodoma.
Mrithi huyo anatafutwa kutokana na kwamba Balozi Nchimbi ameteuliwa kuwa mgombea mwenza katika kupeperusha bendera ya CCM kwenye nafasi ya makamu wa Rais.
Mkutano huo unaowaleta pamoja maelfu ya wana CCM kutoka kila pembe ya Tanzania,utatanguliwa na kusikia utekelezaji wa Ilani ya CCM 2020.
Aidha,baada ya kupokea utekelezaji itafuta Agenda la Ilani ya CCM 2025,ambayo wagombea wa CCM,Mwenyekiti wasasa wa chama hicho na Rais Samia Suluhu Hassan watakwenda kuinadi kwa wananchi kuomba ridhaa ya kuchaguliwa Oktoba mwaka huu.
Rais Samia anaomba nafasi kumalizia kipindi cha miaka mitano baada ya kuingia madarakani mwaka 2021 akitokea kuwa Makamu wa Rais.
Jana, Halmashauri Kuu ya CCM iliwachagua wajumbe wanne wa Kamati Kuu, katika kikao chake maalum kilichofanyika jana Mei 28,2025, jijini Dodoma.
Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni Namelock Sokoine, Dk. Juma Abdallah, Salim Faraj Abri, na Hamad Hassan Chande.
Post a Comment