
DODOMA: Mamlaka ya Ushibiti wa Huduma za Nishati na Maji ( EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta aina ya petroli zitakazotumika hapa nchini kwa mwezi Desemba 2025, zikionesha kuendelea kushuka kwa bei ya petroli.
Ahueni hiyo inatokana na kupungua kwa gharama za kuagiza mafuta katika bandari ya Dar es Salaam kwa wastani wa 2.4% kwa petroli, na 3.6% kwa mafuta ya taa.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule, leo 3 Desemba 2025, imebainisha kuwa, bei ya rejareja ya petroli imepungua kwa shilingi 2.38 (Dar es Salaam), 2.26 (Tanga) na shilingi 2.45 kwa Mtwara. Aidha, bei ya mafuta ya taa kwa Dar es Salaam imepungua kwa shilingi 120.48 ikilinganishwa na bei za mwezi Novemba 2025.
Hivyo basi, bei za reja reja za petroli kwa mwezi huu, zitakuwa shilingi 2610.10, 2616.13 na 2616.24 kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia. Kwa upande wa dizeli, Dar es Salaam ni shilingi 2639.54, Tanga 2648.86 na Mtwara 2654.32. Bei ya mafuta ya taa kwa Dar es Salaam ni shilingi 2513.87 huku bei za Tanga na Mtwara zikiwa hazina mabadiliko kutoka mwezi uliopita.
EWURA inawahimiza wauzaji wa mafuta nchini kutoa stakabadhi za mauzo kwa wanunuzi zinazoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita, kwani stakabadhi hizo hutumika kama kithibiti kunapokuwa na changamoto yoyote kuhusu huduma hiyo.
Aidha, EWURA inavikumbusha vituo vyote vya mafuta nchini kuchapisha bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana yakionesha bei, punguzo na vivutio vya kibiashara. Ni kosa kisheria kutoweka bango linaloonekana katika eneo la kituo na adhabu kali itatolewa kwa mujibu wa sheria kwa atakayekiuka.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment