Na Lydia Lugakila, Misalaba Media
Karagwe
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera limemchagua Rongino Wilbard kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo kwa kipindi cha miaka mitano.
Akisoma matokeo ya uchaguzi huo Desemba 2 2025, Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe, Rasul Shandala, alisema kuwa jumla ya madiwani 32 walipiga kura na hakuna kura iliyoharibika.
Ameeleza kuwa kwa matokeo hayo, Mheshimiwa Longino Wilbard ambaye ni diwani wa kata ya Chanika, atahudumu kama Mwenyekiti wa Halmashauri kwa muda wa miaka mitano ijayo.
Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti, madiwani wamemchagua Mheshimiwa Adirian Kobushoke, diwani wa kata ya Rugu, ambaye pia atahudumu kwa kipindi cha miaka mitano.
Baada ya uchaguzi huo, Mwenyekiti mpya Longino Wilbard na makamu wake Adirian Kobushoke wamesema kuwa watahakikisha wanawatumikia wananchi kwa kuibua na kusimamia miradi mbalimbali ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya ya Karagwe.
Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa, amewasihi madiwani kuendeleza ushirikiano waliokuwa nao awali, akibainisha kuwa mshikamano huo ndiyo msingi wa kusukuma maendeleo katika kata 23 za wilaya hiyo, hususan kwenye sekta za elimu, afya, maji na miundombinu.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Julius Laizer, amewataka madiwani wapya kujifunza kutoka kwa madiwani wenye uzoefu ili kujenga Karagwe yenye dira ya maendeleo na kukuza maendeleo .
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment