" NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

NGAZI YA CHETI NA DIPLOMA KWA MWAKA WA MASOMO 2025/2026

Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwajuma Lingwanda (katikati), akizungumza na waandishi wa habari wakati akitangaza kufunguliwa kwa dirisha la udahili wa Astashahada na Stashahada 2025/2026 katika ofisi za NACTVET Makao Makuu, Mtumba jijini Dodoma

Na.Alex Sonna-DODOMA

BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) limefungua rasmi udahili wa wanafunzi kwa mwaka wa masomo 2025/2026 kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada katika kozi zote zinazosimamiwa na baraza hilo.

Hayo yameelezwa leo Mei 28,2025 jijini Dodoma na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt Mwajuma Lingwanda,wakati akizungumza na wandishi wa habari ambapo amesema kuwa udahili wa wanafunzi umefunguliwa Rasmi kuanzia leo Mei 28 hadi Julai 11 mwaka huu.


Dkt.Lingwanda amesema kuwa maombi ya udahili kwa kozi zisizo za Afya na Sayansi Shirikishi na kozi za Afya na Sayansi Shirikishi zitolewazo katika Vyuo vilivyopo Zanzibar yatumwe moja kwa moja kwenye Vyuo husika kuanzia leo.

Aidha amesema kuwa maombi ya kozi za Afya na Sayansi Shirikishi Tanzania bara yatafanyika kupitia mfumo wa Udahili wa pamoja ( Central Admission System-CAS) unaopatikana katika tovuti ya Baraza hilo kuanzia sasa hadi Julai 11,mwaka huu.


"Kozi zinazoonbwa na vyuo vinavyotoa kozi hizo vimeorodheshwa kwenye kitabu cha mwongozo wa Udahili kwa mwkaa wa masomo 2025/2026 ambao unapatikana katika tovuti ya baraza hilo (www.nactvet.go.tz) kuanzia sasa."

Aidha ameongeza kuwa "Mwombaji anatakiwa kuhusika mwenyewe katika zoezi zima la kuomba kudahiliwa,kuandika taarifa zake kwa usahihi na umakini na kutunza kumbukumbu atakazopatiwa na baraza kupitia namba zake ya simu,bila kumpatia mtu mwingine yeyote ili kuepuka usunbufu katika zoezi zima la maombi ya kujiunga na kozi mbalimbali"

Katika hatua Nyingine Dkt Lingwanda ameweka wazi mambo ya kuzingatia kwa waombaji kupitia mfumo wa udahili wa pamoja yaani (Central Admission systems) akiwemo muombaji anaweza kuomba chuo zaidi ya kimoja hivyo kuchaguliwa katika Chuo alichoomba kutategemea ushindani utakaokuwepo katika chuo hicho.

Aidha Muombaji akishachaguliwa,atapokea ujumbe kutoka NACTVET kupitia namba ya simu yake aliyoweka kwenye mfumo wakati wa kufanya maombi.ujumbe huo utamjulisha kuwa amechaguliwa kujiunga na chuo fulani.

"Baada ya taarifa zake kuhakikiwa,atapokea ujumbe kutoka NACTVET ukimjulisha kuwa amehakikiwa na utakuwa na msimbo (code) ambao atatakiwa kuutumia kuangalia taarifa zake za uhakiki.Pia atatakiwa kuutunza msimbo huo na kuuwasilisha kwa chuo alichochaguliwa siku atakapokwenda katika chuo hicho kwa ajili ya kuanza masomo"amesema Dkt.Lingwanda

Hata hivyo amesema kuwa baada ya kusajiliwa,mwanafunzi anatakiwa aingie katika tovuti ya NACTVET (www.nactvet.go.tz),kisha ajiridhishe kuwa amesajiliwa kwa kuhakiki taarifa zake kwa kubonyeza "link"
inayosomeka "student's information verification"

Post a Comment

Previous Post Next Post