Na
Mapuli Kitina Misalaba
Zoezi la uchukuaji na
urejeshaji wa fomu za kugombea ubunge kupitia Chama cha ACT Wazalendo
linaendelea kwa kasi mkoani Shinyanga, ambapo leo watia nia nane wamerejesha
fomu kutoka majimbo ya Shinyanga Mjini, Itwangi na Kishapu.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Afisa wa Oganizesheni, Mafunzo na Uchaguzi ACT
Wazalendo Taifa, Bwana Risasi Semasaba, amesema kuwa zoezi hilo linaendelea
vizuri katika majimbo yote na linatarajiwa kufungwa rasmi Mei 31, 2025.
Amesema
hadi sasa katika Jimbo la Shinyanga Mjini pekee, watu watano tayari wamerejesha
fomu, jambo linaloonesha mwitikio mzuri wa wanachama na wananchi walioguswa na
ajenda za chama hicho.
Baadhi
ya watia nia wamezungumza mara baada ya kurejesha fomu zao, wakieleza dhamira
yao ya kuleta mabadiliko chanya endapo watapewa ridhaa ya kuipeperusha bendera
ya chama hicho na hatimaye kuwatumikia wananchi kwa uadilifu.
Zoezi
hilo linaendelea katika ofisi za ACT Wazalendo mkoani humo huku viongozi wa
chama hicho wakisisitiza kuwa mchakato huo unazingatia misingi ya uwazi, usawa
na demokrasia.


Post a Comment