" TAWFA YATOA MAFUNZO YA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YA SAMAKI KWA WANAWAKE

TAWFA YATOA MAFUNZO YA KUONGEZA THAMANI YA MAZAO YA SAMAKI KWA WANAWAKE

Mkurugenzi wa shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) Dr Editrudith Lukanga.

Na Mwandishi Wetu, MisalabaMedia

Mtandao wa Wanawake wachakataji Kanda ya Ziwa TAWFA umetoa mafunzo ya uongezaji wa thamani wa mazao ya Samaki Kwa Wanawake kutoka mikoa ya Kagera na Geita.

Mafunzo hayo wamepatiwa na wataalamu kutoka Chuo Cha Mafunzo na Elimu  ya Uvuvi ni pamoja na Uchakataji wa Samaki,Utengenezaji wa Sambusa za Samaki,Ukaushaji Dagaa na   uhifadhi bora wa mazao yote ya  Samaki.

Mratibu wa mradi Tanzania,Lucy Kilanga amesema mafunzo waliyopatiwa Wanawake hao wafanyabiashara wa Samaki yatawasaidia kuongeza mnyororo wa thamani.

"Hivi sasa hapa tunao Wanawake vinara ambao wanatokea mkoa wa Kagera na Geita Kwa hiyo kupitia mradi huu tunawajengea uwezo ili kuongeza mnyororo wa thamani na wao wataenda kuitoa elimu hii Kwa wanavikundi wenzao"alisema Kilanga

Kilanga amesema mradi huu ambao unafadhiliwa na Bill and Melinda Foundation unatekelezwa katika nchi tatu za Kenya,Tanzania na Uganda.

Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) Dr Editrudith Lukanga amewataka Wanawake hao kwenda kushindana sokoni Kwa kuzalisha bidhaa zenye ubora.

Nao wahitimu wa mafunzo hayo Febronia Marwa na Judith Paul wameupongeza Mtandao wa wanawake wachakataji kanda ya ziwa, FETA na EMEDO kwa kuwaongezea ujuzi katika biashara zao na kuahidi kwenda kuwafundisha wanawake wachakataji wengine waliopo katika Vikundi vyao.

Mafunzo hayo ya siku tatu yaliyohudhuriwa na jumla ya wanawake 27 kutoka mikoa ya Kagera na Geita.
Mratibu wa mradi huo Tanzania, Lucy Kilanga akizungumza.

Febronia Marwa mhitimu wa Mafunzo. 



Post a Comment

Previous Post Next Post