" UMEME KUKOSEKANA KESHO SEHEMU KUBWA WILAYA ZA SHINYANGA NA KISHAPU KUPISHA MABORESHO KITUO CHA IBADAKULI

UMEME KUKOSEKANA KESHO SEHEMU KUBWA WILAYA ZA SHINYANGA NA KISHAPU KUPISHA MABORESHO KITUO CHA IBADAKULI

 


 Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Shinyanga limewatangazia wakazi wa mkoa huo kuwa kutakuwa na katizo la huduma ya umeme katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Shinyanga na Kishapu, ili kupisha kazi za maboresho ya miundombinu ya umeme.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja ya TANESCO, maboresho hayo yatafanyika katika kituo kikuu cha kupoozea na kusambaza umeme cha Ibadakuli, ikiwa ni juhudi za kuboresha hali ya upatikanaji wa umeme katika Mkoa wa Shinyanga.

Kwa mujibu wa ratiba ya shirika hilo:

  • Alhamisi, Mei 8, 2025 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, huduma ya umeme itakatika katika maeneo ya Jambo, Jielong, Dahong, Nyanhende, Busongo, Mwadui, El-Hilal, Mwamagunguli, Mayanji, Ukenyenge, Kanawa, Nhobola, Ngunga, Itilima, Muguda, Kalitu, Ngofila, Mhunze, Ndoleleji, Kishapu, Mwamalasa, Mwangongo, Bulekela, Idisa na vijiji vya jirani.

  • Jumamosi, Mei 10, 2025 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni, huduma itakosekana katika maeneo ya Ndembezi, Ndala, Mwawaza, Ngokolo, Mjini kati, Mwasele, Lubaga, Bushushu, Mtaa wa Viwanda, Ibinzamata, Nhelegani, Kizumbi, Ushirika, Kalogo, Maganzo, Buchambi, Songwa, Mwigumbi, Bubiki, Bunambiu, Itongoitale, Wishteleja, Seke, Kabila, Utemini, na viwanda vyote pamoja na maeneo ya Samuye, Usanda, Isela, Tinde, Puni, Zobogo, Kituli, Itwangi, Luhumbo, Didia, Kigwang’ona, Ihalo, Ilola, Lyamidati, Masengwa, Mwakitolyo, Mahembe, Mawemilu, Lyabukande, Solwa, Salawe, Nyandolwa, Kakla, Mwenge, Manigana na vijiji vya jirani.

TANESCO imetoa wito kwa wakazi wa maeneo husika kuwa wavumilivu wakati wa kipindi cha maboresho haya muhimu na imewahakikishia kuwa huduma itarejeshwa mara tu baada ya kazi kukamilika.

Kwa maelezo zaidi, wateja wanahimizwa kuwasiliana na TANESCO kupitia simu ya bure 180.

Post a Comment

Previous Post Next Post