Na: Belnardo Costantine, MisalabaMedia.
Waziri Mkuu wa Kassim Majaliwa, leo ametembelea na kukagua miundo mbinu ya Uwanja wa Benjamin William Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam, kuona ukarabati unaoendelea ikiwa ni maandalizi ya matukio makubwa ya michezo na kitaifa yanayotarajiwa kufanyika hapo.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu alikagua kwa karibu viti vipya vilivyofungwa katika majukwaa ya uwanja huo, pamoja na eneo la kuchezea "pitch" ambalo limeboreshwa kwa kuzingatia viwango vya kimataifa.
Hatahivyo baada ya ukaguzi huo, Majaliwa alieleza kuridhishwa na kasi ya ukarabati na ubora wa vifaa vinavyotumika, akisema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Serikali ya kuboresha sekta ya michezo nchini.
Post a Comment