Na Mapuli Kitina Misalaba
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Angelina Adriano Maganga, tayari amechukua fomu ya kuwania nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Solwa mkoani Shinyanga kupitia chama hicho tawala.
Angelina ameweka bayana dhamira yake ya kulitumikia Jimbo la Solwa ikiwa ni sehemu ya kuendeleza jitihada za maendeleo kwa wananchi, huku akitumia kauli mbiu ya mshikamano, uwazi na maadili ya kiuongozi.
Jimbo la Solwa limekuwa likishuhudia hamasa kubwa ya kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025, huku wanachama mbalimbali wa CCM wakiendelea kujitokeza kuchukua na kurudisha fomu za kugombea.
Kwa sasa macho na masikio ya wakazi wa Solwa yanabaki kwa chama chake kusubiri hatua zinazofuata, huku Angelina Maganga akiwa miongoni mwa majina yanayozua mjadala wa matumaini mapya.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment