
Na Mapuli Kitina
Misalaba
Mwenyekiti wa mtaa wa Ngokolo Mwalimu James
Msimbang'ombe, amefanikisha zoezi la kurejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kuwania
nafasi ya Udiwani katika Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga kwa tiketi ya Chama
Cha Mapinduzi (CCM).
Mwalimu Msimbang'ombe amerejesha fomu hiyo leo Juni
30, 2025 katika ofisi za CCM Kata ya Ngokolo, hatua inayomuweka rasmi kwenye
orodha ya wanachama hai wanaowania uteuzi ndani ya chama kuelekea uchaguzi wa
serikali za mitaa mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Akizungumza mara baada
ya kurejesha fomu hiyo, Msimbang'ombe amesema amejiandaa kwa moyo wa kujitoa na
kwa dira ya kusimamia maendeleo ya kweli kwa wananchi wa Ngokolo.
Zoezi la uchukuaji na
urejeshaji fomu ndani ya Chama Cha Mapinduzi linaendelea katika kata na Wilaya mbalimbali
za Mkoa wa Shinyanga, huku wagombea wakiendelea kujitokeza kuomba ridhaa ya
kuwatumikia wananchi kupitia nafasi mbalimbali za uongozi.
Mwalimu James Msimbang'ombe (kushoto) akikabidhi fomu ya kuwania udiwani kwa Katibu wa CCM Kata ya Ngokolo, katika ofisi za chama hicho leo Jumatatu Juni 30, 2025.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI WAKATI AKICHUKUA FOMU
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment