Na Mapuli Kitina Misalaba
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka Mtaa wa
Maghorofani, Bugweto, Kata ya Ibadakuli, Mwalimu Naomi Kache,
amejiunga rasmi kwenye mchakato wa kuwania nafasi ya udiwani
wa Kata ya Ibadakuli, baada ya kuchukua fomu leo Juni 30, 2025, katika ofisi za CCM kata hiyo.
Naomi amesema amechukua
uamuzi huo kwa dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Ibadakuli kwa
uaminifu, uwazi na uadilifu, endapo chama chake kitampa ridhaa ya kupeperusha bendera
ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao.
Amempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu
Hassan, kwa namna anavyoongoza nchi kwa hekima, busara na
kuhimiza usawa wa kijinsia katika uongozi, Naomi amesema ametiwa moyo na hatua
za Rais Samia kuwaamini wanawake katika nafasi mbalimbali za maamuzi.
Mchakato wa uchukuaji wa fomu ndani ya CCM unaendelea katika kata na Wilaya mbalimbali mkoani Shinyanga kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.
Naomi Kache, kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akipokea fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwania nafasi ya udiwani Kata ya Ibadakuli, Manispaa ya Shinyanga, katika ofisi za CCM kata hiyo leo Juni 30, 2025.
Naomi Kache
Post a Comment