Na Mapuli Kitina
Misalaba
Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Wazazi Taifa kupitia Chama
Cha Mapinduzi (CCM), Hatibu Mgeja,
leo Juni 30, 2025, ameonyesha
dhamira ya kuwatumikia wananchi kwa karibu zaidi baada ya kuchukua na kurejesha
fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho kuwania nafasi ya udiwani katika Kata ya Ngokolo, Manispaa ya Shinyanga.
Hatibu Mgeja
amekabidhiwa fomu hiyo katika Ofisi za CCM Kata ya Ngokolo na kaimu katibu wa
chama kata hiyo.
Akizungumza mara baada
ya kurejesha fomu, Mgeja amesema uamuzi wake wa kuwania nafasi hiyo umetokana
na nia ya dhati ya kuwatumikia wananchi kwa karibu zaidi na kuhakikisha
changamoto zinazowakabili zinapatiwa majibu ya haraka kwa ushirikiano kati ya
uongozi na jamii.
Zoezi la uchukuaji na
urejeshaji fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya CCM
linaendelea maeneo mbalimbali nchini kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Post a Comment