MWANDISHI WETU, TANGA
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Wazalendo Huru Tanzania, Balozi Dkt. Mohamed Mwampogwa, amechukua fomu ya kuwania Ubunge Jimbo la Handeni mkoani Tanga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Dkt. Mwampogwa amechukua fomu hiyo Juni 29, 2025, katika Ofisi ya CCM wilaya ya Handeni ambapo ameeleza kuwa dhamira yake ni kuona wananchi wa Jimbo la Handeni wakipata maendeleo makubwa kupitia utatuzi wa kero zao.
Katika hatua nyingine, Dkt. Mwampogwa amesema amefurahishwa na mapokezi mazuri aliyopata katika Ofisi ya Chama na hivyo kufanikiwa kukamilisha vyema mchakato mzima wa ujazaji na urudishaji wa fomu.
VIilevile, Dkt. Mwampogwa amesisitiza Umoja na Upendo miongoni mwa watia nia wote wa Ubunge Jimbo la Handeni na kwamba yeyote atakayeteuliwa basi washirikiane nae kwani ushindi wa Chama ndiyo muhimu zaidi.
Balozi Dkt. Mwampogwa ni Mwalimu kwa Taaluma, Balozi wa Amani duniani, huku juhudi zake zikitambuliwa ndani na nje ya nchi, kufikia hatua ya kutunukiwa Shahada za Uzamivu za Heshima (PhD) nne katika nyakati tofauti tofauti.
Sambamba na hilo, Dkt. Mwampogwa ni muasisi wa Jukwaa la Wazalendo Huru Tanzania, ambalo limekuwa mstari wa mbele kuchochea ajenda ya uzalendo miongoni mwa Watanzania, utunzaji mazingira, upingaji wa vitendo vya ukatili, rushwa ndani ya jamii.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Post a Comment