Na Mwandishi wetu
Kagera
Evance Emmanuel Kamenge, mchumi na mkulima kutoka Mkoani Kagera, amezungumza kwa kujiamini kuhusu azma yake ya kuchukua fomu ya kugombea kiti cha ubunge katika Jimbo la Missenyi.
Akizungumza katika kipindi cha mchaka mchaka cha redio Kasibante Juni 27, 2025 Kamenge ameeleza kwamba anatarajia kuungwa mkono na chama chake, CCM, pamoja na wapenzi wengi wa chama hicho ambapo wataenda kupima uwezo wao kuelekea uchaguzi Mkuu ujao.
Kamenge Amesisitiza kuwa ana matumaini makubwa ya kufanikiwa huku akiamini kwamba Mungu atamsaidia.
Aidha amewahakikishia wananchi wa Jimbo la Missenyi kuwa, endapo atachaguliwa kama mbunge, atakuwa mbunge wa vitendo na atawajibika kwao kwa njia inayoonekana.
Hata hivyo ameonyesha dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Jimbo hilo endapo atafanikiwa huku vipaumbele vyake vikiwa ni katika uchumi wa uzalishaji.
Ikumbukwe kuwa Juni 28,2025 Kamenge anaenda kuchukua fomu kugombea ubunge wa Jimbo la Missenyi kupitia chama cha Mapinduzi CCM.
Post a Comment