" AHADI YA KAMENGE KWA WANA MISSENYI

AHADI YA KAMENGE KWA WANA MISSENYI


Na Mwandishi wetu, Kagera

Evance Emmanuel Kamenge, mchumi na mkulima kutoka mkoani Kagera, amefanya mahojiano katika redio moja ya Bukoba kuhusu azma yake ya kuwania ubunge katika Jimbo la Missenyi ikiwa Juni 28, 2025 anavuta fomu ya kugombea kiti hicho.

Kamenge ameshukuru wana Missenyi kwa kujitolea na kuchangia fomu yake ya kugombea huku akieleza kuwa msaada wao umempa motisha kubwa kuendelea na safari hiyo hivyo endapo atafanikiwa katika safari hiyo atakuwa mbunge wa vitendo.

Katika mahojiano hayo, Kamenge amesema, “Nitumie fursa hii kuwashukuru wana Missenyi kwani leo, wakati napita katika baadhi ya makundi ya mitandaoni, nimeona hamasa kubwa ambapo watu zaidi ya mia moja walikuwa tayari wamenichangia kiasi kinachohitajika hivyo nitawalipa kwa vitendo"alisema Mwanauchumi hiyo.

Amesema kuwa, ingawa alikuwa na uwezo wa kulipia fomu hiyo mwenyewe, lakini jambo la kuungwa mkono na jamii yake kumemfanya ajisikie mwenye nguvu zaidi.

"Nawashukuru sana siwezi kuwalipia kwa namna yoyote, ila nawaomba mniombee kwa Mwenyezi Mungu," alisema ili safari yangu ikamilike na muone makubwa.

Akizungumzia suala la mamlaka na nafasi za kisiasa, Kamenge alisema, “ukiisoma Biblia vizuri na Qur’ani, utaona mamlaka iliyo duniani huwekwa na Mungu hivyo sisi tuko hapa kutimiza wajibu, lakini Mwenyezi Mungu ndiye atakayeamua nani atakuwa mbunge wa jimbo la Missenyi.”

Aidha amewataka wana Missenyi kuendelea kumuunga mkono katika jitihada zake, huku akiahidi kuwa kama atafanikiwa kuwa mbunge, atakuwa mbunge wa vitendo kwani dhamira yake ni njema kwao.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post