" KAMENGE ATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WANA MISSENYI WALIOMUUNGA MKONO KUMFUATA KUTOKA CHADEMA KUJA KATIKA CHAMA LAKE CCM

KAMENGE ATOA SHUKRANI ZA DHATI KWA WANA MISSENYI WALIOMUUNGA MKONO KUMFUATA KUTOKA CHADEMA KUJA KATIKA CHAMA LAKE CCM

Ndugu wananchi wa Jimbo la Missenyi,Ningependa kuchukua fursa hii kuwashukuru kwa dhati ninyi, wananchi 67 kutoka kata mbali mbali za Wilaya ya Missenyi mliotangaza kuhama kutoka chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema na kuungana nami katika chama cha Mapinduzi (CCM) ni kauli ya Evance Kamenge alipohojiwa na vyombo vya habari baada ya kuonekana ikisambaaa habari wa watu 67 kuitosa chadema kuinenepesha CCM kupitia mitandao mbalibali ya kijamii. Uamuzi wenu ni ishara ya imani kubwa mliyo nayo katika sera na maono ya chama chetu, na ni mfano wa kuigwa katika kuhakikisha tunajenga jamii imara na ya mafanikio kwa ajili ya wana Missenyi "alisema Kamenge.Kamenge amessema kuwa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu anaahidi kusimamia maslahi ya wana Missenyi kwa karibu na kuhakikisha kuwa kila mmoja anapata fursa za maendeleo. "Tunapaswa kushirikiana ili kuleta mageuzi chanya katika sekta zote, ikiwemo mbali mbali ikiwemo Elimu, afya, na miundombinu"alisema Kamenge.Aidha amewaomba Wana Missenyi kuendeleza umoja wao ili waweze kufikia malengo yao ya pamoja.Hii si hatua ya mwisho kwa Evance Kamenge bali ni mwanzo wa safari mpya ya maendeleo na mafanikio makubwa kwa Jimbo la Missenyi.Evance Kamenge  ni mgombea Ubunge, Jimbo la Missenyi Mkoani Kagera na ana matarajio makubwa ya kutwaa Jimbo hilo kutokana na desturi ya Jimbo la Missenyi la kila mbunge kuchukua kwa miaka mitano mitano kisha kuachia ngazi ya kuruhusu wengine kupaa.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

 

Post a Comment

Previous Post Next Post