" KUKAMILIKA KWA DARAJA LA JP MAGUFULI KUMELE TA NEEMA MWANZA

KUKAMILIKA KWA DARAJA LA JP MAGUFULI KUMELE TA NEEMA MWANZA


NA NEEMA KANDOLO MWANZA

KUMALIZIKA kwa ujenzi wa daraja la Kigongo Busisi maarufu kama daraja la Magufuli kutafungua fursa  nyingi za kibiashara katika eneo la Kanda ya Ziwa kwa kuwa usafiri wa magari kutoka sehemu moja kwenda upande mwingine utarahisika.

Hayo yamebainishwa jana Jijini Mwanza kufuatia kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo linalounganisha Ziwa kwa upande wa wilaya ya Misungwi na Sengerema ikiwa na urefu wa zaidi ya kilomita 3.

Afisa Tawala wa Otonde Construction and General Supplies, Elirehema Malewo alisema wao kama wafanyabiashara waliowekeza kwenye ujenzi wa jengo la kitega uchumi mjini Geita wanatarajia kuona eneo hilo linakuwa na kasi ya maendeleo kwani kwa sasa hakuna tena uchelewaji wa kuvuka kwenye daraja hilo.

Alisema kwa sasa uwekezaji kwenye jengo hilo la kiitega uchumi mjini Geita lenye urefu wa ghorofa Tano taasisi za serikali na makampuni binafsi yamekodisha huduma za upangaji kwa kuweka miradi mbalimbali kama vile huduma za benki, ofisi za madini,kumbi za mikutano na sherehe.

Malewo alisema anapongeza jitihada hizo zilizofanywa za kujengwa kwa daraja hilo ambalo ni kiunganishi kinachorahisisha usafiri kati ya upande mmoja wa ziwa na mwingine kwani vyombo vya usafiri vinaweza kupita kwa haraka tofauti na hali ya awali ambapo ilibidi kusubiria kwa muda mrefu.

"Tuna Imani kuwa kukamilika kwa ujenzi wa daraja hilo kutafanya kuwepo kwa mzunguko mkubwa wa fedha katika mkoa wa Geita kwani urahisi wa usafiri ni tija na kichocheo kikubwa kiuchumi" alisema Malewo.

Mkaazi wa Katoro Mkoani Geita Malimi Shelembi alisema kuwa anashukuru kuona kuwa daraja sasa limekamilika hivyo itasaidia kuchochea maendeleo katika eneo lao.


Post a Comment

Previous Post Next Post