Mahakama ya Tanzania imetangaza kuwa mashauri ya jinai namba 8606/2025 na 8607/2025 dhidi ya Tundu Lissu yatasikilizwa Jumatatu, 2 Juni 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam. Mashauri hayo yatarushwa mubashara kupitia mitandao ya kijamii na tovuti ya Mahakama (www.judiciary.go.tz) ili kuruhusu wananchi kuyafuatilia bila kuhudhuria mahakamani.

Ukumbi wa Mahakama utachukua watu wachache tu: Mawakili wa Serikali (10), wa Utetezi (60), na Waandishi wa Habari (10). Wananchi wengine wanahimizwa kufuatilia kesi kupitia mitandao kwa mujibu wa Mpango Mkakati wa Mahakama ya kuimarisha uwazi na matumizi ya TEHAMA.

Matangazo ya moja kwa moja yataanza kabla ya saa 2:30 asubuhi. 

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA