" MHANDISI JAMES JUMBE WISWA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPITIA CCM

MHANDISI JAMES JUMBE WISWA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA SHINYANGA MJINI KUPITIA CCM

Mdau wa maendeleo na mhandisi nguli nchini, James Jumbe Wiswa, leo Juni 28, 2025, amejitosa rasmi katika mbio za kuwania ubunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), baada ya kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho katika ofisi ya CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini.

Mhandisi Wiswa ni miongoni mwa wagombea wapya wanaoonesha nia ya kuwatumikia wananchi kupitia jukwaa la kisiasa, akisisitiza kwamba sasa ni muda wa kuchangia kwa ukaribu zaidi kwenye sera na sheria zitakazowagusa wananchi wa Shinyanga Mjini moja kwa moja.

Mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu ndani ya CCM unaendelea nchi nzima huku chama hicho kikitarajia kupitisha wagombea wake rasmi kupitia mchakato wa vikao vya ndani, kabla ya kuelekea katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu.

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

Post a Comment

Previous Post Next Post