" Mwanamuzi Harmonize Kugombania Ubunge Jimbo la Tandahimba

Mwanamuzi Harmonize Kugombania Ubunge Jimbo la Tandahimba

 

Mwimbaji Staa wa Bongofleva Rajabu Adbul Kahali maarufu Harmonize @harmonize_tz ametangaza rasmi dhamira yake ya kwenda kugombea Ubunge wa Jimbo la Tandahimba Mkoani Mtwara ambako ndio alikozaliwa.

Kabla ya kuongea  na kuthibitisha dhamira yake hiyo, Harmonize aliandika maneno yafuatayo kwenye ukurasa wake wa Instagram “Tandahimba Member of Parliament 2025 Inshallah October ✅ CCM oyee #SamiaMitanotena”

Itakumbukwa October 15,2019, Harmonize ambaye kwa sasa ana-hit na wimbo mpya wa ‘best couple’, alitajwa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli ambaye aliweka wazi kuwa anatamani Mwimbaji huyu akagombee Ubunge wa Tandahimba ingawa kwa wakati huo Harmonize alionekana kutokuwa tayari kugombea kiti hicho.

Hayati JPM alinukiwa akisema ““Lakini nampongeza sana Harmonize sijui anatoka Jimbo gani?, Tandahimba?, Mbunge wa kule ni nani?, (Katani), aah ningetamani sana Harmonize aende akagombee kule awe Mbunge wa Tandahimba”

Akiongea  kwa njia ya simu, Harmonize ambaye alizaliwa Kijiji cha Chitoholi Wilayani Tandahimba Mkoani Mtwara, amesema alichokiandika saa kadhaa zilizopita kuhusu dhamira ya kugombea Ubungo sio kitu cha utani bali anamaanisha ambapo muda ukifika atakwenda kuchukua fomu kupitia CCM ili aombe ridhaa ya Chama hicho kimpitishe kugombea.

Post a Comment

Previous Post Next Post