" Rais Samia Apongeza Bunge la 12 kwa Mchango wa Kisheria na Kisera

Rais Samia Apongeza Bunge la 12 kwa Mchango wa Kisheria na Kisera

 

Na Emmanuel Mbatilo


Serikali imeendelea kutimiza ipasavyo wajibu wake kwa mhimili wa dola wa Kutunga Sheria kwani katika kipindi cha uhai wa Bunge la 12, kulipitishwa miswada 60, maazimio 922, na vilevile Serikali imetoa taarifa 15 kupitia kauli za Mawaziri bungeni kwa ajili ya kutoa ufafanuzi wa masuala yenye maslahi mapana kwa taifa.

Ameyasema hayo leo Juni 27, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati akitoa hotuba ya kuhitimisha shughuli za Bunge la 12 Jijini Dodoma.

"Hakika mmefanya kazi kubwa kwani michango na ushauri wa Bunge hili umekuwa chachu kwa baadhi ya hatua tulizochukua kwenye mabadiliko ya kisera, kisheria na kiutendaji yaliyofanywa na Serikali". Amesema Rais Samia

Amesema Serikali iliongeza kiwango cha Mfuko wa Jimbo kutoka shillingi bilioni 11 mwaka 2021/2022 hadi shillingi bilioni 15.9 kuanzia mwaka 2022/2023 hadi sasa ili kurahisisha utendaji wenu majimboni na kuchochea maendeleo.

"Ni matumaini yangu kwamba fedha hizi mlizitumia vyema katika kuwaletea wananchi maendeleo". Amesema

Post a Comment

Previous Post Next Post