" Serikali haikopi kwa ajili ya mishahara au posho bali inakopa kwa ajili ya maendeleo

Serikali haikopi kwa ajili ya mishahara au posho bali inakopa kwa ajili ya maendeleo

 






 Na Edwin Soko

" Mheshimiwa spika Serikali haikopi Kwa ajili ya kulipa mishahara au posho bali inakopa kwa ajili ya kufanya maendeleo, hivyo kasi ya  kukopa inaendana na Kasi ya maendeleo Nchini"  Hayo yamesemwa na  Waziri wa fedha Mwigulu Nchemba Bungeni Leo Juni 24, 2025 alipokuwa anatoa ufafanuzi juu ya kuongezeka kwa deni la Taifa lililofika Trlioni 107.7.

Waziri Nchemba katika kutoa msisitizo wake mbele ya wabunge juu ya nia chanya  ya Serikali ya kukopa alieleza kwa kutolea mfano wa trilioni 27 za ujenzi wa reli ya mwendo kasi (SGR) Kwa uelekeo wa Mwanza na Kigoma kwa kusema maendeleo kama hayo hayawezi kusubiri miaka arobaini ndipo yakamilike bali mpango sahihi ni kukopa na kujenga kwa muda mfupi na kukusanya faida na kulipa deni.

Nchema pia alisisitiza kuwa, ukopaji mwingine  pia ulifanyika kwenye ujenzi wa Chuo Kikuu cha UDOM, ambapo Kwa sasa watanzania wengi wananufaika na chuo hicho, ikiwemo Utekelezaji wa dhamira ya sera ya elimu ya kuboresha miundombinu ya kujifunzia.

Aliongeza kwa kutoa mfano wa ukopaji na ujenzi wa madarasa na jinsi ulivyosaidia kuondoka  kwa kuchaguliwa Kwa wanafunzi kwa awamu ya pili(Second selection). Pia  ununuzi wa vifaa tiba kwenye dhamira chanya ya kutekeleza sera ya afya ikiwemo Utekelezaji wa sheria ya bima ya afya kwa wote na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Kujitokeza kwa Waziri Mwigulu Nchemba Bungeni na kutoa ufafanuzi wa kuongezeka kwa deni la Taifa na sababu za kuongezeka kunaonesha ukomavu mkubwa kwa chama Cha Mapinduzi na Serikali ya sita.

Hoja zinazoibuka zaidi ni hofu ya  kuongezeka kwa kasi kwa deni la Taifa, hivyo kujitokeza kwa Serikali na kutoa ufafanuzi kunaongeza uelewa Kwa wananchi na kuwa na Imani na Serikali yao.

Huu ni ukomavu mkubwa na utaratibu mzuri sana kwa Serikali kwani kunaleta uwajibikaji baina ya wenye dhamana ya uongozi na watoa dhamana.



Post a Comment

Previous Post Next Post