" TAASISI NUNUZI ZASHAURIWA KUZINGATIA SHERIA KANUNI NA MIONGOZO

TAASISI NUNUZI ZASHAURIWA KUZINGATIA SHERIA KANUNI NA MIONGOZO

  


Na. Eva Ngowi na Chedaiwe Msuya – WF Arusha

Taasisi Nunuzi zashauriwa kuzingatia sheria, kanuni, miongozo iliyowekwa kwa mujibu wa sheria na kuwa na maadili ili kukomesha mambo ambayo ni kinyume na matarajio ya Serikali. 

Hayo yameelezwa na Kamishna wa Sera ya Ununuzi wa Umma, Dkt. Frederick Mwakibinga wakati wa Kongamano la tisa la Ununuzi wa Umma la mwaka 2025 linaloendelea katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha. 

Alisema kuwa uzingatiwaji wa Sheria utaweza kupunguza kiwango cha upotevu wa mali na kuchukua hatua ambazo zimewekwa katika Sheria ili kukomesha mambo ambayo ni kinyume na matarajio ya Serikali na kuhakikisha kwamba fedha za umma zinalindwa kadiri inavyowezekana. 

“Kama mnavyofahamu ununuzi wa umma ni moja kati ya nyenzo zinazotumika kwa manufaa mbalimbali ikiwemo kuutumia ununuzi wa umma kwa kuzinufaisha kampuni za wazawa ili ziweze kukua na kuwa na mchango katika maendeleo ya nchi, kuyajali makundi mbalimbali ya jamii ambayo yakiachwa bila kusaidiwa au kuwezeshwa yanapata ugumu katika ushindani wa soko la ununuzi wa umma.” Alisema Dkt. Mwakibinga


Dkt. Mwakibinga alisema, kongamano hilo muhimu limekutanisha, Wadau wa Ununuzi wa Umma kwa maana ya Watendaji wa Umma, Makampuni, Viongozi, Wafanyabiashara na watu mbalimbali ili kufanya majadiliano ya kujenga himaya ya Ununuzi wa Umma iliyo thabiti. 


Kongamano hilo limeandaliwa na Mamlaka ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma- PPRA, iliyobeba dhima ya “Ununuzi wa umma kidijitali kwa maendeleo endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi maalumu kwa ukuaji wa Uchumi jumuishi. 



Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Dkt. Frederick Mwakibinga, akizungumza kwenye mdahalo wakati wa Kongamano la tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, lililofanyika katika Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Kamishna wa Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Dkt. Frederick Mwakibinga (katikati) na Maafisa Ugavi, Bi. Jamila Byekwaso (wa pili kulia), Bw. Raphael Chima (wa kwanza kulia), Bi. Vaileth Mwakajisi (wa pili kushoto) na Bi. Beatrice Zenda (wa kwanza kushoto), kutoka Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi” lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Baadhi ya Washiriki kutoka Taasisi mbalimbali wakifuatilia Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi” lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.

Afisa Ugavi  Mwandamizi kutoka Idara ya Sera ya Ununuzi wa Umma, Wizara ya Fedha, Bi. Jamila Byekwaso akizungumza na  Mkaguzi wa Ndani kutoka Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania, (TLSB) Bi. Rukia Amini wakati alipotembelea Banda la Wizara katika Kongamano la Tisa la Ununuzi wa Umma la Mwaka 2025, lenye kauli mbiu “Ununuzi wa Umma Kidigitali kwa Maendeleo Endelevu: Ukuzaji wa Kampuni za Wazawa na Makundi Maalum kwa Ukuaji wa Uchumi Jumuishi”, lililofanyika katika Ukumbi wa Kituo cha Kimatifa cha Mikutano (AICC) jijini Arusha.


(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Arusha)

Post a Comment

Previous Post Next Post