Edwin Soko
Kampuni ya Barrick nchini yenye ubia na Serikali kupitia kampuni ya Twiga Minerals inawajengea uwezo wachimbaji wadogo wapatao 1800 kwenye mgodi wa North Mara.
Hayo yamebainishwa na Neema Ndosi toka kitengo Cha habari Cha Kampuni ya Barick alipokuwa anawasilisha mada juu ya ,mafanikio ya Barick kwenye warsha ya siku moja Kwa wahariri wa habari toka Vyombo mbalimbali Nchini.
Ndosi alibainisha kuwa, Barick inatambua uwepo wa wachimbaji wa wadogo kwenye mgodi wa North Mara hali iliyopelekea kuamua kuwajengea uwezo wachimbaji hao kwenye maeneo mbalimbali kama vile elimu ya uchimbaji wa madini, na elimu ya fedha ili wafanye kazi zao kwa ufanisi kama sera ya madini ya Mwaka 2009 inavyosisitiza.
"Hatua hii ina imarisha mahusiano baina na menejimenti ya Barick na jamii inayozunguka mgodi wa North Mara hali inayoimarisha ulinzi na usalama" Aliongeza Ndosi.
Hatua hii pia inaaksi Utekelezaji wa sera ya madini ya Mwaka 2009 inayosisitiza kwenye kuwatambua wachimbaji wadogo na kuwajengea uwezo na kuwatambua.
Wasilisho hilo pia ililieleza mafanikio kwenye maeneo mbalimbali ya kisera na kisheria yanayotekelezwa vyema na Kampuni ya Barrick kama vile uhifadhi wa mazingira na uongezaji wa thamani katika nyanja za elimu na afya.
Naye Damas Makangale, Mwandishi wa habari na mshiriki wa warsha hiyo alieleza kuwa, Jitihada za Barrick kwenye kuimarisha mahusiano mazuri na Vyombo vya habari itasaidia shughuli za Barrick kuandikwa zaidi na kufanya jamii ielewe vyema mchango wa Barrick katika uwekezaji wa sekta ya madini unaofanywa na Barrick Kwa ubia wa Serikali.
Naye Meneja Mkazi wa Barrick Nchini Tanzania Daktari Melkiory Ngido alipopata nafasi ya kuwasalimia washiriki alisisitiza juu ya nafasi ya Vyombo vya habari kwenye kutoa elimu kwa umma juu ya mchango wa Kampuni ya Barrick kwenye ukuaji wa uchumi wa Nchi kupitia ulipaji wa Kodi na utoaji wa ajira Kwa watanzania .
Daktari Ngido aliongeza kuwa, Kwa miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mtazamo chanya wa picha ya Kampuni ya Barrick katika utekelezaji wa shughuli zake tofauti na huko nyuma. Hali hii inatokana na kazi nzuri inayofanywa na Vyombo vya habari hapa nchini.
Warsha hiyo ya siku moja ilifanyika kwenye makao Makuu ya Barrick Jijini Dar es salaam na kujumuisha waandishi wa habari ambao ni wahariri toka kwenye Vyombo vya habari mbalimbali hapa Nchini.
Kampuni ya Barrick kwa sasa inaendesha shughuli zake kwenye migodi miwili, North Mara na ule wa Bulyanhulu huku ikiwa kwenye hatua za mwisho wa kufunga mgodi wake wa Buzwagi ambao shughuli zake zilishasimamishwa.
Post a Comment